Sunday, March 29, 2009

MWAKYEMBE ALISTAHILI KUJITOA KAMATI YA RICHMOND


Ninachouliza ni hiki, la Dr. Harrison George Mwakyembe tunatoa hata nukuu kuwa kwa kuwa yeye ni mzalendo, basi tufumbie macho pale palipoonekana wazi kuwan COI. Infact tumefikia hatua ya kuanza kuulizana maana ya COI na kuleta utaalamu wa kutambua maana ya COI, huku ukweli ni kuwa alichokifanya kwa macho mepesi, pamoja na kuwa laonekana kuwa limetuondesha janga, linaingia madoa kwa kuwa yeye mwenyewe Mwanafyale Mwakyembe ana hisa katika kampuni inayotarajia kufua umeme.

Narudia tena, kujadili kwetu suala ma mwakyembe ni wazi kuwa tunaamka na kutoendelea kufumbia macho mambo kisa ushabiki na mapenzi yetu kwa mtu.

Mfano, pamoja na kuwa mimi ni shabiki wa Nyerere, nakubali wazi kuna mambo aliyoyafanya hayakuwa ya tija wala hayajaleta manufaa kwa Taifa letu. Sasa kama ningekuwa nimekunywa mkorogo wa fenesi na papai, ningesema Nyerere hajawahi kufanya makosa na ni mtakatifu daima.

Sasa Mwakyembe ni ama alifanya kwa makusudi au kujenga mazingira ya kufumbia macho dhamana aliyopewa ya kuchunguza mradi wa umeme uliopewa kwa mshindani mwenzake (yes it is a fellow competitor mtake msitake) huku yeye mwenyewe akiwa anajijengea maslahi na uwanjwa wa kuwa na uwezo wa kupiku na kuuza umeme kwa Taifa. Alichofanya yeye kadai kulia uzalendo na uchungu wa uzawa!

Kama tunataka kujenga jamii na Taifa bora ambalo tunalilia siasa safi, uongozi bora na maadili, basi ni shurti tuachane na kufumbia macho kupindishwa kwa sheria na kanuni kunakofanywa na vipenzi vyetu.

Revolutionary Right Reverend Kishoka

No comments:

Post a Comment