Wednesday, April 28, 2010

MKUTANO WA KUJADILI ANDIKO LANGU

Siwezi sibitisha endapo itakuwa kweli, lakini leo hii limetolewa tangazo katika Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Mzumbe na Mkuu wangu wa Idara ya Katiba na Sheria za Utawala (Constitutional and Administrative Law) Bw. Ignas Seti Punge kwamba, Mkutano wa kujadili na kuitolea hoja na mapendekezo andiko langu la Kuanzisha Kituo cha Msaada wa Sheria Chuo Kikuu Mzumbe (Starting a Legal Aid Clinic at Mzumbe University) utafanyika Mei 3, 2010 yaani siku ya Jumatatu ijayo.

Tarehe hiyo ni mara tu baada ya sikukuu ya Kimataifa ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) na kabla tu ya Mgomo wa nchi nzima wa Wafanyakazi walio Chini ya Muungano wa Vyama Vya Wafanyaklazi, TUCTA. Kuna Vyama 13 vilivyo chini ya TUCTA. Muda unanikwamisha kuvitaja vyama hivyo papo kwa papo, lakini baadhi yake ni kile cha Vyuo Vikuu [RAAWU], TUGHE (Serikali Kuu na Afya), TALGWU, TUICO, TEWUTA, CHODAWU, n.k.

Habari zaidi baada ya kufanyika mkutano huo kutoa mrejesho hapa, inshallah.