Thursday, April 25, 2013

376 CATTLE DISAPPEAR FROM RUVU RANCH TANZANIA [JULY 2012 - MARCH, 2013]

Posted here on 25th April, 2013. 

 From the Guardian, Tanzania, 23 April, 2013
376  COWS DISAPPEAR !   SHAME  ON US!   THIS IS PUBLIC PROPERTY!

A total of 376 cows are reported to have disappeared mysteriously from Ruvu Ranch in Coast Region, betweem july, 2012 and March, 2013, police have confirmed.
The disappearance of the animals is contained in a letter dated April 2 this year that the general manager of the National Ranching Company (NARCO), Dr John Mbogoma, sent to the Permanent Secretary in the Ministry of Livestock Development and Fisheries.

The letter said the cows disappeared from the ranch between July last year and March this year.

"In a normal inspection conducted in the ranch by the internal auditor on February 27, 2013, it was discovered that 304 cows had vanished. The figure was obtained from the January 1, 2013, count,” the letter said.
It said following the count, the NARCO management formed a probe team to conduct an inquiry from July last year to March 6, this year.

Apart from the loss, the letter said a monthly report showed that Ruvu Ranch was leading in the deaths of cows which occurred in October last year.
"The loss was discovered to have occurred every month since July 2012, but it was not reported to the ranch authorities,” the letter said.
The confidential letter said that following the strange disappearance of the animals, the NARCO management reported the matter to the Chalinze police station on March 22, leading to the arrest of the suspects.
The case has been transferred to the Coast Region police headquarters for further investigation, the letter said.

Coast Regional Police Commander Ulrich Matei said police are still conducting investigation on the case.

He said the investigation is being carried out by experts from the police force, the Tanzania People’s Defence Force, the Prevention and Combating of Corruption Bureau, the Tanzania Intelligence Services, the Immigration and the Prisons.
He said the aim is to use the expertise of every organ in crime fighting.
"We also want transparency in our investigation because the issue seems big requiring joint efforts.” he said.
"What I can only say is that investigations are continuing. I don’t want say where we have so far reached.”

Wednesday, April 24, 2013

MAREHEMU PROFESA MICHAEL WAMBALI [UDSM] AAGWA !

Imetundikwa hapa tarehe 24/4/2013

KWA  HERI  MWALIMU WETU  PROFESA  MICHAEL  WAMBALI

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, na wakili maarufu Profesa Michael Wambali ambaye alifariki dunia Aprili 4, 2013 katika hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye ajali ya gari.


Shughuli ya kuuaga rasmi mwili wa marehemu Profesa Wambali ilifanyika leo asubuhi (Jumatatu, Aprili 8, 2013) kwenye ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla ya kupelekwa kanisani kwa misa maalum.
Akizungumza na waombolezaji hao kabla ya kutoa heshima za mwisho, Waziri Mkuu alisema mchango wa Prefesa Wambali kwenye fani ya sheria ni mkubwa mno na hauelezeki. “Kama walimu wenzake wangeamua kuhesabu idadi ya wanafunzi ambao Profesa Wambali aliwafundisha, ni dhahiri kuwa idadi yao ingekuwa kubwa kuliko tunavyoweza kufikiria,” alisema.
“Juzi tu tarehe 29 Machi, ametimiza miaka 59 ya kuzaliwa na siku sita baadaye akaaga dunia, lakini katika kipindi cha miaka yake 59 ni miaka 32 ambayo aliitumia hapa chuoni. Hapa tulipo wapo Majaji, Mawakili wa Serikali na wa kujitegemea, mahakimu na wengine wako mikoani wameshindwa kufika hapa leo… lakini wote hawa wamefundishwa na Prof. Wambali katika kipindi cha miaka 32 aliyokaa hapa chuoni,” alisema.
Alisema fani ya sheria imepoteza kiongozi makini na mfano wa kuigwa. “Tumepoteza kiongozi mzuri na makini siyo kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam peke yake bali ni kwa Tanzania yote,” aliongeza.

Aliwasihi wanafamilia waikubali hali ya kuondokewa na mpendwa wao, wajipe matumaini kwamba mwenzao ametangulia na akawataka waendelee kumuombea kwa Mungu ili ampokee huko mbinguni.

Kwa wanafunzi wa wafanyakazi wa Shule Kuu ya Sheria, Waziri Mkuu alikuwa na haya ya kusema: “Ingawa Profesa Wambali ameondoka, ninaamini bado ataendelea kuwa nasi kwani ametuachia kazi zake nyingi za kimaandishi ambazo zitatumiwa na wengine katika siku zijazo. Tukienzi hilo, tutakuwa tunaendeleza yale aliyokuwa akiyasimamia.”

Naye Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dk. Asha-Rose Migiro ambaye aliwahi kufanya kazi na Profesa Wambali miaka ya 80, wakati akitoa nasaha zake alisema alifanya naye kazi ofisi moja na waliwahi kufundisha masomo ya aina moja.



Dk. Migiro alisema kila aliyewahi kuwa mwanafunzi wa Prof. Wambali hawezi kuacha kumkumbuka. “Hatuwezi kumrudisha kwa sasa ila kila aliyewahi kuwa mwanafunzi wa Profesa Wambali atamkumbuka daima. Mike ameondoka lakini atabakia mioyoni mwetu. Kila tutakapoona familia yake ama kuona kuona kazi zake za taaluma, tutaendelea kuonana naye,” alisema.



Waziri Mkuu amewasili mjini Dodoma mchana huu kuhudhuria mkutano wa 11 wa Bunge unaotarajiwa kuanza kesho (Jumanne, Aprili 9, 2013).     Mimi alinifundisha somo la "EVIDENCE"  pale  Mlimani  mwaka  1996/97 (mwenye blogu)

Thursday, April 18, 2013

ON MARGARET THATCHER'S [FORMER UK CONSERVATIVE PARTY PRIME MINISTER] PASSING

On Margaret Thatcher’s Passing


by John Andrews / April 10th, 2013

I’m just a tiny, tiny bit sad today.

So, Thatcher’s dead. I live in the town where she was born and raised. There are inevitably some who are in deep mourning today, and a few little bunches of flowers have appeared outside the corner shop that was her first family home. On the other hand, there’s also quite a bit of celebrating, and I was speaking to a woman today who said she just hopes that Cameron and Osborne and all the rest of them do the decent thing and jump onto her funeral pyre. Given the fact that her home town, once well-known for its heavy industry, is now largely silent because of Thatcher’s policies, you can see her point.

For myself, I must confess that a very tiny part of me is sad. Whilst she still breathed there was a miniscule theoretical possibility that she could be held to account for the vast crimes against humanity, in general, and the British people, in particular, that were committed by her government. I’m truly sad that even that miniscule theoretical possibility has been permanently snuffed out.

Three years into her reign a poll published in the Times revealed that she was the most unpopular British prime minister in history. And then things got worse.

She began by causing the deaths of a thousand people over a clump of wind-blown rocks 8,000 miles away from Britain, supposedly to defend the right of 2,000 people to call themselves British. It would have been cheaper for this supposed champion of democracy and devotee of Chicago-school economics to pay for those people to move lock, stock and barrel to the UK, accommodate them and give them all Income Support for the rest of their lives, than to wage a war and support a military garrison on the Malvinas to the end of time. But that little fact is always conveniently overlooked.

Thatcher’s foreign policies had one striking feature in common: her government’s support of murderous dictatorships was total; and the line-up of tyrants who enjoyed the backing of her government is quite impressive. There was Pol Pot, for example, and the unspeakable Suharto in Indonesia. Everyone knows about the blood-soaked Pinochet whose evasion from justice was actively assisted by Thatcher’s government. Less well known about are the assortment of Middle-Eastern despots her government aided; but the daddy of them all, the most ruthless oppressor on the face of the Earth, the US government, was always Thatcher’s favourite; and she made significant contributions to its goal of world domination. It’s impossible to know how many tens, if not hundreds of thousands of unnecessary deaths were aided and abetted by Thatcher’s government.

Impressive though her foreign policies obviously were, they pale to insignificance compared with the treacherous actions of her government against the British people. Her mission from the outset was to kill-off the trade union movement which, for all its imperfections, was the only real champion the ordinary Briton had. Once that was done it was game over, lambs fattened and ready for slaughter. She proceeded to kill-off the main source of Britain’s wealth, our manufacturing base; and then rapidly sold off every bit of family silver she could get her hands on. In quick succession Britain’s essential publicly owned utilities were flogged at fire-sale prices: transport, water, electricity, communications, gas… all went under the hammer. Millions of jobs were trashed or scrapped altogether, and then she turned her attention to the last remaining protection the British people had: public services. Why did she do all this? Just so a tiny, tiny handful of obscenely wealthy people could become even more obscenely wealthy.

What a great legacy. You can see why people want to put up statues to her.

The economic wasteland that Britain is today is not all Thatcher’s fault: others followed her who could have put things right, but didn’t. Nevertheless, it was Thatcher who started the ball rolling.

There was never any real chance that Thatcher would have to account for her crimes, but I am truly sad that the miniscule theoretical possibility that she could have been brought to justice is now gone forever.

Tuesday, April 16, 2013

HAKIELIMU's (NGO) VIEWS ON THE 2013/2014 TANZANIAN BUDGET !!!


Imetundikwa hapa leo hii tarehe  16/4/2013.

TAMKO LA HAKIELIMU KUHUSU

BAJETI YA SEKTA YA ELIMU MWAKA WA FEDHA 2013/2014

 
UTANGULIZI

Yanayotokea sasa katika sekta ya elimu yanaleta aibu kusimulia na yanaumiza kutafakari. Uwezo duni wa vijana wanaohitimu shule za msingi na sekondari, wanafunzi kufaulu bila kujua kusoma na kuandika, kuporomoka kwa ufaulu na kuongezeka kwa kiwango cha kutojua kusoma na kuandika ; haya ni baadhi tu ya mambo ambayo yanapaswa sasa kutufumbua macho na kutufanya tutambue ukweli kuwa tunapoteza mwelekeo na kama hatua za makusudi za kunusuru elimu zisipochukuliwa, basi tujue tunajenga taifa la watanzania wasio na ujuzi na maarifa ya kutatua changamoto za kiuchumi, kisiasa na kijamii zinazoendelea kutukabili.

Hali hii imeshaanza kuathiri upatikanaji wa maendeleo ya mtu binafsi, familia na hata taifa kwa ujumla. Tumepuuza kwa muda mrefu hali ya kushuka kwa ubora wa elimu, leo hii tunashuhudia matunda yake na kama tutaendelea “kufunika kombe mwanaharamu apite” tutajifariji na uwepo wa wanafunzi shuleni lakini wasio jifunza kikamilifu wala kuelimika ipasavyo, hatimaye kuwa na taifa mbumbumbu ambalo litashindwa kujiongoza.

Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne mwaka 2012 yanaakisi kiwango cha juu cha kudorora kwa elimu nchini na matokeo ya kuipuuza elimu. Tumeshuhudia watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wakipata daraja SIFURI katika matokeo hayo; 103,327 sawa na asilimia 26.02 wakipata daraja la nne huku wanafunzi 23,520 tu, ambao ni sawa na asilimia 5.16 (waliopata kati ya daraja la kwanza, la pili na la tatu) ndiyo wakihesabiwa kufaulu vizuri.

Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la saba mwaka 2012 hali kadhalika, sehemu kubwa ya waliochaguliwa (zaidi ya wanafunzi 294,833) wamepata ufaulu wa daraja “D”. Aidha, zaidi ya watahiniwa 139,923 sawa na asilimia 35.45 ya waliofanya mtihani wa kitaifa wa kidato cha pili 2012, hawakufaulu. Kiwango cha kutojua kusoma na kuandika kinazidi kuongezeka na sasa kimefikia asilimia 30 tofauti na ilivyokuwa miaka ya 1980 ambapo ilikuwa asilimia 9 tu. Wanafunzi wengi wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma na kuandika.

Takwimu za elimu hadi mwaka 2012 zinaonesha hali ya mazingira ya kujifunzia katika shule zetu kuanzia elimu ya awali mpaka sekondari kutokuwa ya kuvutia. Uwiano wa mwalimu mwenye sifa kwa mwanafunzi kwa elimu ya awali umebaki kuwa 1:124 badala ya 1:25; uwiano wa matundu ya vyoo kwa wanafunzi msingi unakadiriwa kuwa 1:56 badala ya 1:25 kwa wavulana na 1:55 badala ya 1:20 kwa wasichana. Mrundikano wa wanafunzi darasani ni mkubwa mno, wastani kwa nchi nzima ni 1:70 badala ya 1:40, uhaba wa madawati unafikia asilimia 49.1 kwa sasa ikiwa ni upungufu wa takribani madawati 1,879,806 kati ya 3,893,338 yanayohitajika.
Shule za sekondari pia zinaathiriwa na changamoto za namna hii ikiwa ni pamoja na tatizo la uhaba wa mabweni, maabara, vitabu na walimu wa masomo ya sayansi. Pia hamasa ya mioyo ya walimu kujitolea na kuridhika na ualimu iko chini sana(HakE, 2011). Changamoto hizi zinatupa ishara kuwa shule zetu za umma (msingi na sekondari) si shule ambazo zina viwango vya kuridhisha na hata kumsaidia mwanafunzi afundishwe na ajifunze ipasavyo.

Siyo siri kuwa changamoto hizi zina uhusiano wa moja kwa moja na upangaji wa vipaumbele vyetu na maamuzi ya matumizi ya rasilimali za taifa. Ikiwa tunataka kutoka hapa tulipo kwenda mahali bora zaidi ni lazima upangaji wa bajeti katika sekta ya elimu uangaliwe kwa makini sana kwa kuwashirikisha wadau wote wa sekta ya elimu ili kutatua changamoto za sekta ya elimu. HakiElimu inaishauri serikali sasa kuacha visingizio vya uhaba wa bajeti na wahisani kukwamisha utekelezaji wa mipango ya kuikwamua elimu. Kwa kutambua mchango wa ushiriki wa wadau na HakiElimu tukiwa wadau tunaosononeshwa na hali mbaya ya elimu inayoendela kwa sasa, yafuatayo ni maoni au mapendekezo ya HakiElimu katika upangaji wa bajeti ijayo ya sekta ya elimu 2013/2014. Na haya tungependa yatiliwe mkazo sana;-
TATIZO LA WANAFUNZI KUTOJUA KUSOMA NA KUANDIKA

Hili bado ni tatizo kubwa na hadi sasa serikali haijawa na mkakati maalumu wa kuondoa tatizo hili. Shule za msingi kwa madarasa yote bado zina wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika. Hali hii imejitokeza pia katika baadhi ya shule za sekondari licha ya serikali kudai itawabaini na kuwaondoa. Tatizo hili lazima lianze kufanyiwa kazi kwa kuwa na mpango maalumu wa kutathmini idadi kamili ya wanafunzi hao na kupanga mkakati wa makusudi wa kutokomeza tatizo la kuwa na wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika sekondari. Mpango huu lazima uwashirikishe wadau wote wa sekta ya elimu hasa wazazi na kamati za shule ili watambue majukumu yao katika kuondoa tatizo hili.

Kwa kuwa elimu ya awali ni msingi wa mwanafunzi katika kujifunza kusoma na kuandika, tunataka kuona bajeti hii inatia mkazo katika uwekezaji katika elimu ya awali hasa kuwa na walimu bora na vifaa vya kujifunzia na kufundishia. Uwekezaji katika elimu ya awali utachangia sana kupunguza tatizo sugu la kuwa na wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika katika shule za msingi. Tunatambua kuwa katika Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM III), Serikali imeazimia kuanzisha fungu maalumu katika bajeti ya elimu (separate budget line) kwa ajili ya elimu ya awali na kutenga asilimia 20 ya matumizi yake ya kawaida kwa ajili ya sekta ya elimu huku asilimia 60 ya fedha zitakazotengwa kwa ajili ya sekta kuelekezwa katika elimu ya awali na msingi. HakiElimu ingependa kuona mpango huu ukianza kutekelezwa kikamilifu katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2013/14.

UHABA WA FEDHA NA WATAALAMU IDARA YA UKAGUZI WA SHULE

Ripoti ya tathmini ya Mpango wa pili wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM II) inaonesha kutofikiwa kwa malengo ya ukaguzi wa shule hivyo kuziacha shule nyingi bila kukaguliwa. Sababu kubwa ya kutofikiwa kwa malengo ya ukaguzi ni uhaba wa fedha unaosababisha uhaba wa vitendea kazi na wataalamu wa ukaguzi. Mwaka 2011/12 shule za msingi zilizokaguliwa ni 3,061 tu kati ya 7,200 zilizopangwa kukaguliwa (sawa na asilimia 42.5). Aidha, sekondari 935 (43.3%) zilikaguliwa kati ya 2,100 zilizopangwa kukaguliwa. Hii ni kusema ni asilimia 19.1 pekee kati ya shule za msingi nchini hukaguliwa na asilimia 21.4 tu ya sekondari hukaguliwa kwa mwaka. Tafsiri hapa ni kuwa uwezo wa fungu la ukaguzi katika bajeti ni kukagua asilimia 20 tu ya shule zake zote, asilimia 80 ya shule hazipati fursa ya kukaguliwa kutokana na uhaba wa bajeti.

Athari za shule kutokaguliwa ni nyingi, kwa mfano utendaji wa walimu kutopimwa, utekelezaji wa mitaala, maendeleo ya shule na wanafunzi kutopimwa. Kama ukaguzi haufanyiki kwa nini tunashangaa wanafunzi kufeli au kumaliza elimu ya msingi na kufaulu mitihani ilihali hawajui kusoma na kuandika? HakiElimu inatoa rai katika bajeti ya 2013/14 kutoa kipaumbele katika kuimarisha ukaguzi wa shule. Serikali itenge fungu la kutosha kwa ajili ya ukaguzi, tumeona athari ya shule kutokaguliwa katika matokeo mabaya ya wahitimu wa darasa la saba, kidato cha pili na cha nne 2012 na tusingependa kuona haya yakijirudia.

SERA YA ELIMU NA MAFUNZO NA SERA YA ELIMU YA AWALI

Serikali imeendelea kupanga bajeti zake kwa kuzingatia “Sera ya Elimu na Mafunzo iliyopitwa na wakati” (ETP 1995). HakiElimu inajiuliza Mpango wa III wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM III) ambao serikali imeanza kuutekeleza umetokana na sera gani? Pia Mabadiliko ya mtaala wa elimu kutoka kuwa Mtaala unaoangalia maudhui kwenda katika Mtaala unaomjengea mwanafunzi ujuzi ulifanywa kwa kutumia sera gani? Je imetumia sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 au rasimu ya sera mpya ambayo bado haijapitishwa?

Tunahoji sera gani kwa kuwa sera ya 1995 inayopigiwa kelele kutokidhi mahitaji na kupitwa na wakati haijapatiwa mbadala na ni wazi kuwa kuendelea kupanga bajeti kwa kutumia sera iliyopitwa na wakati kunaweza kusitupe matokeo mazuri yanayokusudiwa katika elimu kama ambavyo tumeshuhudia katika matokeo ya kidato cha nne 2012. Wakati umefika sasa waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi aje na majibu juu ya lini sera hii itakuwa tayari na itaanza kutumika ili kutoa dira katika mipango na utelekelezaji wake ikiwemo bajeti.

UHABA WA FEDHA ZA RUZUKU SHULENI

Ili kuinua ubora wa elimu, serikali iliazimia kutoa ruzuku kwa kila mwanafunzi kupitia MMEM na MMES Shilingi 10,000 kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi na 20,000 kwa mwanafunzi wa sekondari kila mwaka. Hata hivyo, takwimu za elimu 2012 zinaonesha wastani wa sh. 6,025 tu ndizo hufika shuleni badala ya 10,000/= kwa shule za msingi na wastani wa shilingi 14,178/= pekee badala ya shilingi 20,000/= zilizoahidiwa kwa kila mwanafunzi wa Sekondari.
Hali hii imekwamisha shughuli nyingi za maendeleo ya wanafunzi shuleni, vitabu havinunuliwi kwa wakati, nyenzo za kufundishia na fedha za uendeshaji wa shule hazitoshi. HakiElimu inaishauri serikali kutenga kiwango kamili cha 10,000/= na 20,000/= kama mipango inavyoonesha. Na tena ni muhimu upangaji uzingatie mfumuko wa bei ambao umekuwa ukiathiri pia uwezo wa shilingi katika kufanya manunuzi, itakumbukwa kuwa upangaji wa kiwango hiki cha ruzuku ulifanyika 2002-2006 wakati mfumuko wa bei ukiwa katika wastani wa 4.4% wakati leo wastani wa mfumuko wa bei ni asilimia 14.9% , hii ni mara tatu zaidi ya kiwango cha awali.

UPANGAJI NA USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA

Serikali imekuwa ikitoa ahadi juu ya kupunguza bajeti ya matumizi ya kawaida kwa muda sasa, (Hotuba ya Waziri wa Fedha Juni 9, 2011). Hata hivyo bado Wizara ya Elimu imeendelea kutenga fedha nyingi katika matumizi ya kawaida huku eneo la “matumizi mengineyo” likiendelea kutengewa fedha nyingi zaidi. Takwimu zinaonesha bajeti ya matumizi ya kawaida ya wizara imeongezeka kutoka bilioni 523.8 mwaka 2011/12 hadi bilioni 631.9 mwaka 2012/13, sawa na ongezeko la asilimia 20; wakati fedha za matumizi mengineyo (posho, mafuta, safari, samani na ukarimu) ikiongezeka kutoka bilioni 207 mwaka 2011/12 hadi bilioni 386 mwaka 2012/13 sawa na ongezeko la asilimia 86. Hii ina maanisha bado agizo na ahadi ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima halizingatiwi katika bajeti zetu.

Pia utekelezaji wa bajeti ya sekta ya elimu umekuwa si mzuri. Licha ya serikali kudai haina fedha za kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu, bado kumekuwa na usimamizi mbaya wa hata zile fedha kidogo zinazopangwa. Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2010/2011 imebainisha fedha zilizotolewa kwa miradi ya MMEM na MMES kushindwa kutumiwa na Halmashauri katika kutekeleza miradi hiyo. Hata fedha zinazotolewa kwa ajili ya mfuko wa jimbo ambazo zingesaidia kuboresha shule zetu nazo hazitumiki.

Rai yetu ni kuwa bajeti hii ya mwaka wa fedha 2013/14 iachane na matumizi ya kawaida yasiyokuwa ya lazima, badala yake fedha hizo zitumike kutatua changamoto muhimu kama vile urekebishaji wa maslahi ya walimu kama mishahara, posho za mazingira magumu, nyumba katika maeneo yasiyokuwa na nyumba za kupanga na kuboresha mazingira yao ya kufundishia shuleni. Hatua hii itasaidia kurudisha morali wa ufundishaji na kupunguza matatizo ya ufaulu nchini. Upangaji wa fedha na matumizi yake katika elimu kamwe hauwezi kuwa na mafanikio iwapo kutaendelea kuwepo kwa kutoelewana kati ya walimu na serikali. Mwalimu ni mtekelezaji mkuu wa bajeti na mipango shuleni, hivyo hakuna budi kukawa na maelewano kati ya wadau hawa muhimu ili utekelezaji wa mipango uwe na ufanisi na uwekezaji ulete tija.

Pia, tufike mahala sasa tupange bajeti kwa kuwa na vipaumbele vichache ili tuvitekeleze. Ni dhahiri kuwa, Serikali haiwezi kutatua matatizo yote kwa wakati mmoja, hivyo lazima tujenge utamaduni wa kuwa na kipaumbele au vipaumbele vichache katika bajeti kwa kila mwaka wa fedha ili kutatua changamoto za sekta ya elimu. Bajeti hii lazima ieleze bayana mikakati ya Wizara ya kuboresha usimamizi na ufanisi wa fedha za umma hasa katika kuhakikisha fedha zinafika kwa walengwa kwa wakati, zinatumika kama zilivyopangwa na zinatumika ipasavyo kwa mantiki ya kuleta ufanisi wa fedha.

Elizabeth Missokia

Mkurugenzi Mtendaji
HakiElimu

Sunday, April 14, 2013

FAIDA ZA MTI WA MLONGE [MORINGA]

 Imedakwa toka mitandaoni, leo hii 14 Aprili, 2013.

 FAIDA  ZA  MTI  WA  MLONGE  [MORINGA]

KAMA kuna mti wenye faida nyingi za kiafya, basi Mlonge unaweza kuwa unaongoza. Kila eneo la mti huu, kuanzia majani, maua, mbegu, magamba  hadi mizizi yake ina virutubisho vya kipekee vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu.

Majani ya Mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wake unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika moja lijulikanalo kama Trees For Life, majani ya Mlonge yana Vitamin A nyingi kuliko karoti, vitamin C nyingi kuliko machungwa na madini ya Potassium nyingi kuliko ndizi mbivu, halikadhalika ubora wa protini yake ni bora kushinda maziwa na mayai.

Kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini ya chuma  (Iron), kasiamu (Calcium) na vitamin nyingi za aina mbalimbali, majani ya mmea huu yamekuwa yakitumika kama ‘tonic’ kwa watoto wadogo na vijana ili kuimarisha mifupa na kusafisha mfumo wa damu mwilini.

Ili kutengeneza ‘tonic’, saga majani mabichi ya Mlonge pamoja na maji, yachuje kisha changanya na maziwa halisi. Inaelezwa kuwa juisi ya aina hii ni dawa nzuri kwa waja wazito, kwani huboresha njia ya uzazi na kumuwezesha mama kuzaa bila matatizo na kuondoa matatizo baada ya kujifungua.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, mti wa Mlonge unatibu karibu magonjwa 300 ya aina mbalimbali, yakiwemo yale magonjwa sugu, baadhi yake ni kama haya yafuatayo:

Mlonge unaweza kutibu Pumu, Kikohozi na Kifua Kikuu. Aidha, magonjwa mengine kama Kisukari, Shinikizo la damu (la juu na chini), magonjwa ya ngozi, magonjwa ya kwenye njia ya mkojo (UTI) kuongeza kinga ya mwili (CD4) na kuongeza nguvu za kiume.