Kutoka kwa Dr. Wilbert Bunini Manyilizu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Tanzania.
Aspartame
Imegunduliwa kuna watu wanaoepuka sukari nyingi katika vinywaji, sasa kuna kemikali inayotumika badala yake, tofauti kidogo na soda ya coca cola iliyozoeleka, kemikali hiyo ni aspartame, ambayo ina madhara mengi zaidi ya tisini kiafya kwa mtumiaji. Unaweza kuona aspartame imeandikwa kwenye kijalada cha karatasi ya Cocacola (Coca zile za kuchanganya na maji), ikiwa imewekewa nyota* kama ingredient. Ukiona kipaketi cha cocacola kimedondoka njiani basi okota uangalie ingredients kwani ingredients huwa haziandikwi kwenye chupa za kuvunjika. Au nunua kinywaji cha Cocacola kilicho kwenye paketi uangalie ingredients, utaona Aspartame*. Aspartame ina athari nyingi kwa afya ya mtumiaji. Madhara ni pamoja na kansa za ubongo, kuzaa watoto wenye ulemavu, kupata ugonjwa wa kisukari, matatizo ya kisaikolojia, na kifafa. Soda hii inapotunzwa muda mrefu katika mazingira ya joto, aspartame hubadilika na kuzaa kemikali zingine hatari kwa afya ya mtumiaji (hizi ni methanol, formaldehyde, formic acid). Kwanza hubadilika kuwa methanol, hii ni mfano wa pombe ambayo ni sumu.
Kuna watu walishaijaribu kuinywa pombe hii ya methanol katika maabara kwa kudhani ni sawa na pombe zingine ambazo ni za aina ya ethanol wakaishia kuwa vipofu. Methanol hii huibadilisha formaldehyde kuwa tindikali ya fomiki (formic acid). Hizi zote mbili zina asili ya kusababisha kansa katika mwili wa mtumiaji.
Kuna aina mbalimbali ya vinywaji vya cocacola ambazo zina kemikali inayoitwa aspartame hii ina madhara mengi ( kama kuanguka kifafa).
Mengine ni; kupungua kwa kinga dhidi ya magonjwa, kupata mfadhaiko wa akili (depression), kukasirika bila sababu za msingi na kuwa na tabia ya kubadilikabadilika (mood swings). Kupoteza kumbukumbu, kukosa usingizi, kujisikia kuchanganyikiwa, kujisikia mwenye hofu bila sababu, kuwa na hisia za kujiua, mwili kufa ganzi, ini kushindwa kufanya kazi vizuri. Madhara mabaya zaidi ni uwezekano wa kupata kansa kutokana na kemikali hii. Inasemekana kiwango cha madhara kinachoweza kutokea kutokana na matumizi ya vitu vinavyotokana na coke ni sawa na yale yanayotokana na uvutaji sigara.
Japo kuna madhara kiafya hakuna anayeshtuka na kuamsha watu kujilinda na hatari hii inayowazunguka kila siku. Ni hakika kuwa watumiaji wakubwa wataishia kunenepa, na kuharibikiwa afya, mfano, kupata kisukari. Lakini pia wasomaji wasidhani kuwa vinywaji vingine vyenye sukari nyingi ni salama kuvikimbilia, kama vile pepsi, fanta nakadhalika kwani viungo vyake haviko mbali na vile vya coke.
No comments:
Post a Comment