Kutoka JamiiForums.
moto wateketeza hoteli mbili bagamoyo
livingstone club: imenusurika oceanic bay hotel: imeteketea yooooote
paradise resort:imeteketea yooote hata foronya haikuwahi kuokolewa
KATIKA KUFUATILIA KWA KARIBU BALAA LA MOTO HUKO BAGAMOYO, GLOBU YA JAMII INAPASHA KWAMBA HOTEL ZA PARADISE NA OCEANIC BAY (PICHANI) ZIMETEKETEA KABISA NA MOTO.
KWA BAHATI HAKUNA MTU ALIYEJERUHIWA ILA INADAIWA HASARA INAKADIRIWA KUWA YA MAMLILIONI YA SHILINGI.
SHUHUDA WA GLOBU YA JAMII ALIYEKO HUKO AMEHABARISHA SASA HIVIKWA VODA KWAMBA MAJENGO YOTE YA HOTELI YA PARADISE YAMETEKETEA NA KWAMBA HAWAKUWAHI KUOKOA HATA FORONYA AMA GODORO AMA UFAGIO.
HALI KAMA HIYO IMEREKODIWA PIA KATIKA HOTELI YA OCEANIC VIEW, AMBAYO NI JIRANI NA PARADISE, ILA YA LIVINGSTONE CLUB, AMBAYO PIA JI JIRANI KWA UPOANDE KWINGINE, IMENUSURIKA KABISA. INASEMEKANA HII NI KWA SABABU YA UPEPO WA BAHARI KUPEPERUSHA MAKUTI KUELEKEA OCEANIC HOTEL
AMESEMA KWAMBA MOTO HUO, ULIOANZA ASUBUHI, ULIDUMU KWA MUDA WA DAKIKA 15 TU NA HOTELI ZOTE MBILI ZIKAWA ZIMETEKETEA. YAANI FAYA AMBAO WALIKIMBIA TOKA DAR KWENDA BAGAMOYO KWA KASI ZOTE WAMEKUTA MAJIVU TU. PICHA KIBAO ZAJA MUDA SI MREFU UJAO..
No comments:
Post a Comment