Toka kwa Alhaj Yusuf Mtingwa Kalala
Zama za Ukoloni na kipindi kifupi baada ya Uhuru nadhani, palikuwa
sheria iliyowalazimisha Wabunge kusema bungeni kwa lugha ya
Kiingereza tu. Ilikuwa patashika kubwa, sipati kukwambia!
Sasa "wasomi" kwa kutaka dunia hii ya "vijisenti" iwe yao peke yao
wanaweka masharti ya "darasa" katika kila "uwanja." Binafsi siioni
mantiki ya "usomi" wa Form IV. Hususan hii ya UPE.
Masharti yasiyokuwa ya msingi, ndio hayo yanayosababisha hizi PhD
za Pacific University na certificates za kughushi na mambo mengine
mengi yasiyokuwa ya lazima. Zipo fani zinazohitaji "usomi" wa kweli
na ujuzi wa uhakika. Lakini si kila mahali.
Chambilecho cha Kikwete, "Hakuna shule ya U-Rais." Churchill na Tony
Blair wa Uingereza wamelithibitisha hili katika kukalia kiti cha Uwaziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment