Saturday, March 21, 2009

GHARAMA ZA UMEME ZINAVYOTUMALIZA WATANZANIA

20/03/2009, James MmM <jamesfrequent@gmail.com> wrote:
....Is this true ?
Note fwd message:
Ndugu zangu napenda kushirikiana nanyi katika kutafakari ni kwa muda gani tutaendelea kupumbazwa na hawa mafisadi. Na tuangalie gharama ambazo TANESCO wanapaswa kuyalipa makampuni mbalimbali kwa ajili ya capacity charge tu. Nimejaribu kuzidisha hesabu alizozitaja Dr. Mwakyembe (kama ziko sahihi) na kupata jumla kuu kwa mwaka.

Kampuni Gharama kwa siku *30 Gharama kwa mwezi *12 Gharama kwa Mwaka
IPTL 103,700,000 *30 3,111,000,000 *12 37,332,000,000
Aggreco 62,000,000 *30 1,860,000,000 *12 22,320,000,000
APR MWANZA 76,000,000 *30 2,280,000,000 *12 27,360,000,000
Dowans 158,000,000 *30 4,740,000,000 *12 56,880,000,000
Songas 265,000,000 *30 7,950,000,000 *12 95,400,000,000
Jumla &nb sp; 239,292,000,000 (kwa kiswahili ni billioni mia mbili therasini na tisa, million mia mbili tisini na mbili )

Hizo ndio gharama TANESCO wanapaswa kulipa kwa mwaka. Sasa najuiliza kwa uchumi upi wa Tanzania wa kuingia gharama zote hizo? hapo bado hujaweka gharama za kununua huo umeme wenyewe, vipuri na mafuta au gesi ya kuendeshea hiyo mitambo. Miradi ya wakati wa crisis inageuzwa ya muda mrefu, hivi tutaondokana na umaskini sisi? TANESCO wanakusanya shillingi ngapi kwa mwaka mpaka waingie gharama zote hizo? Mapato kwenye madini yetu yatalipia hizo gharama? viwanda navyo je vinazalisha kiasi cha kuweza kufidia hizo gharama? Isije ikawa pesa ya wakulima ambao hata umeme kwao ni ndoto ndio inagharamia miradi yote hii. Wanatuambia umeme wa magenereta ni wa emergence ili kufidia pengo lililopo lakini hakuna mradi wowote mkubwa na wa bei nafuu unaotekelezwa kwa sasa ili watuambie labda mwaka 2012 shida ya umeme itakuwa imekwisha baada ya mradi huo kukamilika. Tunachokiona ni kusuasua miradi yote nyeti mfano ni stigler's gorge project ambao upo kwenye makabati miaka nenda rudi, bali ile ya kukombea mabilioni ikiibuliwa kila kukicha. Na wananchi tutaamka lini ili huu upuuzi ukomeshwe?

No comments:

Post a Comment