Tuesday, March 10, 2009

MAONI JUU YA VYAMA VYA UPINZANI TANZANIA

Kuwa CCM ni provider, umelenga nyundo sawasawa juu ya msumari.

CUF, CHADEMA, TLP, NCCR-M na UDP vyote vinategemea zaidi
ruzuku ya serikali ya CCM. Ndio maana wanachama wengi wa vyama
vya upinzani, mimi nawaita ni mashabiki. Hawana "commitment" yoyote
ya michango kifedha.

Matawi yote hulalamikia kutopewa ruzuku na Makao Makuu. Wao
wenyewe hawana chochote wanachopeleka Makao Makuu. Nakumbuka
wakati TANU ilipoanza. Kila mwanachama alilazimika kulipa thumni moja
kila mwezi na makusanyo yote yakipelekwa Makao Makuu ambayo nayo
iliwajibika kutoa mgao kwenye matawi yake.

Nilikwenda kwenye tawi la CUF pale kwetu Kigogo. Ningezubaa wangenitoa
upepo. Shida yao kubwa ilikuwa Makao Makuu haitusaidii kifedha. Nilipouliza
kama wao wanapeleka michango yao ya Shilingi 100 ya kila mwezi. Majibu
yalikuwa hakuna anayetoa michango hiyo, hawana kitu. Nikawauliza, asiyetoa
kitu atapataje kitu? Wakabaki vinywa wazi. Nikawaambia kuwa wao ni mashabiki
wa CUF na si wanachama. Mwanachama huji-commit na commitment yao ni ile
michango ya kila mwezi, kwa udi na kwa uvumba.

Vyama vyenyewe havina miradi ya EPA wala Vitambulisho. Viwanja vyote vya
CCM na walinzi wa magari usiku ni Sungusungu wa CCM - Our Provider.

Mzee Kalala.

No comments:

Post a Comment