Maana ya shule (au elimu) ni kinachosalia kichwani baada ya kusahau yote uliyofundishwa darasani.
Ilitokana na hoja kwamba kuna Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo sasa, aliyewahi kuwa hausigelo (housegirl) wa Mhindi Bukoba.
Tuangalie picha kubwa ya mambo (ze big picture)
Kwanza hakuna uhakika kama huyu Mama (sasa Mbunge) alikuwa hausigelo. Huenda hizo habari ni mikingamo kama zile zinazotoka kwenye blogu ya "Ze Utamu"
Kufuatana na taarifa alizobandika DM, huyu Mbunge alimaliza kidato cha nne mwaka 1976 (kama vyeti vyake siyo batili).
Hatuwezi kuupuza elimu ya Kidato cha Nne (au elimu yeyote) kufuatana na definitions tunazotaka kutumia.
Mifano uliyotoa ya miaka ya 1948 (darasa la 10) naielewa.
With all due respect, dunia imebadilika kwa kiasi kikubwa (hali kadhalika Tanzania).
Kuna mambo mengi hapa duniani yanayohitaji "formal education" .
Kuna mambo mengi kule Tanzania yanayohitaji uelewa wa "formal" education..
Kama huyu Mbunge alikuwa hausigelo mwenye elimu ya darasa la sabna au kidato cha nne cha mwaka 1976, au alikuwa hausigelo wa Mhindi au Mwarabu ....that is not my point.
Maswala yanayohitaji utaalamu maalum, tuwateue wataalm wenye huo utaalam maalum kufanya hizo kazi.
Wataalam wanahujumu nchi (wezi, mafisadi, etc.) wachukuliwe hatua za kisheria za nchi
Mimi inanishangaza kuwa tunapiga porojo za kununu mitambo chakavu ya Kampuni "iliyotuingiza mjini" (kutuhujumu).
Hi yenyewe (hujuma) ni sababu tosha za serikali KIZIRA/TANESCO kununua mitambo hiyo (as a matter of principle) hata kama mitambo hiyo haina dosari.
Tatizo kubwa linalokabidhi taifa siyo wataalamu au utaalam, ila HUJUMA, WIZI, KUTOKUWAJIBIKA, UZEMBE, UFISADI ...na misamiati mingine iliyoko ncje ya upeo wangu wa kujieleza.
Wataalam kibao (tena wenye maadili) wamerudi huku nyumbani lakini hakuna anayewatumia au anayetaka ushauri wao (kwa mfano Mchilyi ni mchumi mahiri ambaye amewahi kufanya kazi na kamati za UN, Inginia Madete kutoka Ujerumani ana ujuzi usio na kifani, na wengine wengi tu).
Kuna hatari (perception or otherwise) au labda tunataka kutumia hili swala ya hausigelo kumfanya Mbuya aonekane kuwa hawadhamini wasiokuwa na PhD kama yeye (NB: sikuzungumzii wewe binafsi Mzee mwenzangu - Meku Kalala. I am not that stupid. (Nimewahi kuona watu waliojikojolea na kusingizia kuwa mvua imewanyeshea ndiyo maana wameloa au kutaka tuamini hivyo)
This is narrow thinking of missing the big picture and getting fixated on a narrow single issue.
Swala la vyeti batili siyo geni ......limefika hata kwenye baadhi ya vyuo vyetu vikuu.
Tumekuwa hata na msamiati mpya wa "kusafisha vyeti" (huko Chuo Kikuu cha Malawi). ....whatever that means.
This is a serious issue my friends. Kama baadhi ya Maprofesa wetu na Wabunge wako katika hizi kashfa za vyeti batili, unatarajia akina "Kalubandika na Pwagu" watetewe na nani?
Ati banda la kuku linalindwa na vimburu au mweha....then the outcome obvious (upungufu wa kuku kila kukicha ...mwishowe banda (Tanzania) litakuwa halina kitu.
Halafu tunashangaa? Wenye akili timamu watatushangaa kwani nini tunashangaa.
As I have said several times (and I am repeating now): THERE IS NO RIGHT WAY OF DOING WRONG.
And for the record:
Mahausigelo wetu ni WAAMINIFU kuliko baadhi ya viongozi na wataalam wetu..
Hatuwezi kujenga Taifa kwa porojo na mzaha ninaouona nchini kwetu.
Mbuya is there/here to defend honest housegirls (wahudumu wa ndani) na wataalam/viongozi waaminifu.
Ukiona mbwa mlizi anaanza kuwang'ata watoto wa nyumbani, basi ujue muda wa kumpiga "shaba" umewadia (metaphorically speaking).
And the time is now.
Tutazungumzia hizi kashfa za Dowans, IPTL, Radar, Richimonduli (na nyinginezo) kwa miaka mingapi ? ....bila hatua za kimsingi.
No comments:
Post a Comment