Friday, March 6, 2009

KIWANDA CHA CHUMA KUJENGWA LUDEWA

Mwandishi Tumsifu Sanga, ilikuwa ukamilishe kiu ya wasomaji kwa kuwafahamisha kuwa hii wilaya ya Ludewa ipo katika mkoa gani Tanzania. Ni kazi yetu waandishi wa habari kuhakikisha kuwa tunachokiandika kisomwapo na mwandishi, hakiachi maswali ya kawaida kama haya.

MWANANCHI
Mach 3, 2009
Na Tumsifu Sanga
SERIKALI imetenga eneo la kujenga kiwanda cha kuzalisha chuma ghafi katika
wilaya ya Ludewa, ambacho ujenzi wake utagharimu takriba Dola 100 milioni za
Kimarekani (zaidi ya Sh130 bilioni za Tanzania).

Kiwanda hicho, ambacho ujenzi wake umepangwa kuanza hivi karibuni, kitaweza kutoa ajira kwa watu wanaokadiriwa kuwa 4,000.

Mbunge wa jimbo la Ludewa, Raphael Mwalyosi alisema hayo wakati alipokuwa
akizungumza na wakazi wa Ludewa waishio jijini Dar es salaam jana kuhusu
mafanikio aliyoyapata katika kipindi cha miaka mitatu ya ubunge.

Alisema kuwa kujengwa kwa kiwanda hicho kumewafanya watenge eneo la hekta
78 kwa ajili ya kujenga Chuo cha Ufundi (Veta) ambacho kitajengwa jirani na
kiwanda hicho kurahisisha wanafunzi watakaosoma katika chuo hicho kufanya
mitihani yao kwa vitendo kiwandani hapo.

“Tayari tumempata mkandarasi wa kujenga kiwanda hicho ambacho kitakuwa ni
kiwanda cha kwanza kwa ukubwa nchini Tanzania na Afrika nzima,” alidai
Mwalyosi Kiwanda hicho kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha chuma ghafi
330,000 kwa mwaka.
Mwalyosi alisema kuwa mbali na ujenzi wa kiwanda hicho pia wameshatenga
maeneo yanayofaa kwa utalii na ujenzi wa mahoteli.

No comments:

Post a Comment