Monday, March 23, 2009

SIASA ZA KUTENGENEZA SILAHA ZA VITA MAREKANI

Tarehe 19 Machi, 2009, katika masomo yetu ya wiki moja Chuoni Emory, Atlanta, tulipewa somo lililoitwa "War, Terrorism and Social Injustice". Mwalimu wetu siku hiyo alikuwa Profesa Barry Levy.

Mwalimu huyu aliniacha hoi alipokuwa anaelezea siasa za Utengenezaji silaha za kivita nchini Marekani. Bwana huyu alisema kuwa kila Jimbo nchini kwake linashabikia sana juu ya utengenezaji huu wa silaha za kivita kwa sababu ifuatayo:

1. Kwamba, kila jimbo la Marekani linachangia kifaa kimojawapo katika kutengeneza hizo silaha. Kwa sababu hiyo, Kila Mbunge atashabikia jambo (yaani atahakikisha linapita bungeni) hili akifahamu fika kwamba watu wa jimboni mwake watafaidika katika ajira ya kutengeneza kifaa hicho. Kwa maana hiyo, kuna faida ya maendeleo itakayopatika katika kila jimbo katika utengenezaji wa silaha za kivita. Wakati huo, hapendwi mtu hapo atakayedhurika na silaha hizo bali waheshimiwa wabunge hao wanahesabu ni Dola kiasi gani zitakazoingia majimboni mwao katika kutengeneza silaha hizo.

Swali ni Je, kwa mtaji huu, kuna siku itakayokuja huko baadaye ambapo Wamarekani watasema jamani tuache vita na kutumia mazungumzo katika kuleta amani ya dunia? Wao wakale wapi? Shughuli inaanzia hapo!

Kwa ukosefu wa muda, sikujaaliwa kumuuliza mtaalam huyu endapo hili pia limo katika sheria za marekani kutumia utaratibu huu au ndio ushabiki wa kisiasa tu.

No comments:

Post a Comment