Saturday, March 28, 2009

MTANZANIA ATUMIWA KUFUNDISHA ELIMU YA BIASHARA MAREKANI

Chuo Kikuu cha Colombia nchini Marekani, kinatumia historia ya Mtanzania, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hoteli za Peacock, Joseph Mfugale kufundishia wanafunzi wa shahada ya uzamili. Mfugale, ambaye ana aelimu ya darasa la saba, pia ni mmiliki wa hoteli za Peacock zilizopo Dar es Salaam zilizoajiri takribani Watanzania 215, na anajenga nyingine yenye hadhi ya nyota tano mjini Iringa. Akizungumza Dar es Salaam jana, Mfugale alisema mwaka jana wataalamu wa chuo hicho walifanya utafiti wa historia za wajasiriamali ili kufahamu walipotoka na namna walivyofanikiwa na katika utafiti huo, walivutiwa na historia yake na kuamua kuingizwa kwenye mitaala ya chuo hicho.

“Kwa hiyo sasa kuna mitaala inayohusu Peacock katika chuo kikuu cha Marekani, mtaji wangu ulitoka kwenye nguvu zangu,” alisema Mfugale na kuongeza kuwa yeye si mkopaji mkubwa katika benki au taasisi za fedha, hajawahi kufanya kazi serikalini na anaamini kwamba mtu yeyote akiamua kufanikiwa anaweza. Mfanyabiashara huyo alisema jana kuwa, wajasiriamali wengi nchini hawafanikiwi kwa kuwa hawana nidhamu katika kufanya biashara na kuwashauri waache matumizi yanayozidi mapato yao.

“Nawaambieni biashara ni nidhamu na kujituma katika biashara…biashara yoyote inaweza kukufikisha unapotaka, usianze kutumia kuliko kiasi unachopata,” alisema na kuongeza kwamba, anaandika kitabu kuhusu historia yake ili wajasiriamali wengine wajifunze na pia wakitaka ushauri kwake yupo tayari kuwasaidia. “Nilipata shida sana katika maisha yangu mpaka nilipofika,” alisema Mfugale na kubainisha kwamba Chuo hicho kimemtumia cheti kutambua mafanikio yake.

2 comments:

  1. Kwanza nianze kwa kukupongeza,blog yako nzuri sana inamambo mengi ya kujifunza nilikuwa siifahamu leo ktk kuperuzi,peruzi ndio nimeifuma sio siri imenivutia sana.

    Sasa kaka na mimi ni mjasiliamali mdogo naomba nikuulize,huyo Mpangule hana web.site yake? kama anayo unaweza kunipatia? naona nina mengi ya kujifunza kutoka kwake.Natanguliza shukrani zangu, kwako asante sana.

    ReplyDelete
  2. Ndugu passion4fashion,

    1. Mwenye blogu hii ni mwanamke, hivyo ni dada.

    2. Mpangule anayo website yake. naomba Ugugo jina la hoteli yake yaani peacock tanzania naona utapata taarifa zake huko.

    ReplyDelete