Saturday, June 19, 2010

MAJIBU YA KUKATISHATAMAA BINAFSI NA KITAASISI

KUJENGA NCHI NI KAZI, NA NI KAZI KUBWA SANA.

Hatimaye baada ya kuelezea ugumu wa mimi kufanya mambo mawili kwa pamoja yafuatayo; ambayo yote yalihitaji muda na kujitolea kwangu kwa bidii yangu yote, yaani:

1. Kuandaa Mabadiliko ya Andiko (Proposal improvement) la kuanzia Kituo cha Kutoa Msaada wa Sheria Chuo Kikuu Mzumbe

2. Kukazania kusoma sana kutayarisha andiko la kwanza kwa masomo ya Digrii ya Uzamivu (PhD Proposal rectification and modification).

Niliandika barua kwa Mkuu wangu kuomba kwamba Jambo la kwanza likabidhiwe kwa mtu (watu wengine) kwa sababu nimetingwa sana na jukumu la pili ambalo tayari nilikuwa nimechelewa (time-barred).

Mkuu wangu wa Kazi akanifahamisha tarehe 14/6/2010 kwamba kwa kuwa hakushirikishwa katika jambo hilo tangu mwanzo, yeye hawezi kufanya lolote. (Wakati nalifanya jambo hili, yeye alikuwa masomoni, na pia kila barua niliyoandika juu ya suala hili niliinakilisha ofisini kwakwa kwa taarifa). Hii maana yake ni kwamba dhamira yangu ya kukienzi chuo changu kwa kufungua kituo kama hicho imekufa kifo cha MENDE.

Hivi sasa nahaha sana kuhangaikia shule yangu ambayo nikifanikiwa nayo, inshaallah, sijakata tamaa, nitaendelea na jambo hilo Na. 1 hapo juu hata kama italazimika kufanya hivyo nje ya Taasisi yangu niliyodhamiria kuwa kianzishwe hapo. Mungu anajua yote, amin.

MAJAJI WAMEPOTOKA RUFAA YA SHAURI LA MGOMBEA BINAFSI

Dk Mwakyembe: Majaji wamepotoka
Friday, 18 June 2010 23:01
Imeandaliwa na Fidelis Butahe, Hussein Issa, Geofrey Nyang'oro na Freddy Azzah
Chanzo : Gazeti la Mwananchi 18/6/2010.

NI KWELI WATANZANIA WANASHERIA WOTE TUNAJIULIZA MAHAKAMA YA RUFAA NI YA KAZI GANI KAMA SIO KUAMUA HAKI ZA WATU KAMA ILIVYOAINISHWA KATIKA IBARA YA 107A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977???


WANASIASA na wasomi nchini wamesema kuwa majaji saba waliotoa hukumu ya mgombea binafsi wamepotoka na kujichanganya kwa kuliachia Bunge jukumu hilo.

Alhamisi, tarehe 17/6/2010 Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilitupilia mbali uwezekano wa kuwepo kwa mgombea binafsi licha ya Mahakama Kuu kuamua katika kesi iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila kuwa sheria inayozuia mgombea binafsi inakiuka Katiba ya nchi.

Kutokana na hali hiyo Mahakama ya Rufaa imerudisha hoja hiyo bungeni ambapo katika hukumu yake ilieleza kuwa suala hilo lazima liwekwe na Bunge ambalo lina uwezo wa kisheria wa kufanya marekebisho ya kikatiba na si mahakama ambazo hazina uwezo huo kisheria.

Mbunge wa Kyela, Dk Harison Mwakyembe ndiye amepinga vikali suala hilo na kusema kuwa haikustahili kupelekwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa.

Alisema yeye kama mwanasheria anafahamu kuwa suala hilo ni la haki, kilichotakiwa kutolewa na mahakama ni mwongozo kwamba nini Bunge linatakiwa kufanya, kwa sababu mahakama ndio inayosimamia sheria badala ya Bunge kuzitunga na kuzipitisha.

"Nikisema suala hili la mgombea binafsi sio haki nikiwa kama mwanasheria, wenzangu na hata wanafunzi wangu watanishangaa sana, ukweli ni kwamba ni haki ya kuwa na mgombea binafsi, ila haina manufaa kwani hawana nguvu, mfano Marekani wanao wagombea binafsi, lakini hawafahamiki," alisema.


Mwakyembe ambaye alisema hayo katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo chaTBC jana asubuhi, aliongeza kuwa mahakama ni zao la katiba, hivyo kilichotakiwa ni kusimamia katiba kama ilivyotungwa na Bunge na sio kurudisha tena majadiliano bungeni badala ya kumaliza kesi hiyo.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye kitaaluma ni mwanasheria, Dk Sengondo Mvungi alisema maamuzi ya mahakama hiyo yameiidhihirishia dunia kuwa Tanzania haiheshimu haki za msingi za binadamu na utawala bora.

"Uamuzi wa jana (juzi), ulimaanisha kuwa Watanzania wote tumepoteza, tumeipoteza miaka zaidi ya 48 ya kupigania uhuru, utawala bora na kuheshimu haki za binadamu," alisema Dk Mvungi ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya katiba.

Dk Mvungi aliendelea kufafanua kuwa, makosa ya Bunge na serikali ya kutomtambua mgombea binafsi, kisheria yalipaswa kurekebishwa na mahakama.

Mvungi alifafanua kuwa, haki za msingi za binaadamu, zilikuwepo tangu siku ya kwanza aliyoumbwa na kuongeza kuwa mahakama inapaswa kulizilinda haki hizo za kiasili.


"Haki za binadamu hazijaundwa na dola wala katiba, mahakama wamekopeshwa tuu kulinda haki hizi, katika utawala bora mahakama lazima iwe na mamlaka ya asili ya kulinda haki za binadamu, kitu ambacho hawa waheshimiwa walikisahau," alisema na kuongeza;

"Kwa hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo imedhihirisha kuwa Tanzania katika suala la utawala bora na kuheshimu haki za msingi za binadamu iko nyuma sana, katika hili mahakama imejipiga risasi yenyewe wala hakuna aliyeishinikiza na imejipotezea heshima yake mbele ya wananchi,".

Naibu Katibu Mkuu wa CUF upande wa Zanzibar, Juma Haji Duni alisema kwa hatua hiyo ya Mahakama ya Rufaa imeonyesha kuwa kwa sasa wananchi hawana mahali pa kupata haki zao za msingi.

"Kama Mahakama na Bunge vimeshindwa kuwasaidia wananchi sasa sijui watakimbilia wapi, unapoona nchi nyingine zina machafuko usidhani kuwa yameanza siku moja, machafuko hayo yanatokana na wananchi kuelemewa na mambo kama haya,"
alisema Duni.

Duni alidai kuwa wananchi wameshavulimilia kwa muda mrefu kukaa bila kupata haki zao za msingi na kwamba hivi sasa wamechoka na hatma ya nchi iko mikononi mwao.

Alidai uamuzi wa mahakama hiyo ulikuwa na shinikizo la serikali na CCM.

Duni alisisitiza kuwa, duniani nzima Mahakama na Bunge vinatakiwa kulinda haki za binadamu na kuwa kwa Tanzania vyombo hivyo vimeshindwa kutimiza majukumu yake hayo ya msingi.

Kwa upande wake mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chadema , Halima Mdee alisema kuwa kesi ilitakiwa iishe kwa mujibu wa sheria na si kuipelekea Bunge kwa kuihusisha na siasa.

Alisema anachokifahamu yeye kama mwanasheria mahakama ni mlinzi wa matakwa ya watu.

"Hili sio suala la kisiasa zaidi kwani kila mtu analifahamu kilichokuwa kinatakiwa hapa ni kutoa maelezo kwa Bunge tu lifanye nini ,"alisema Mdee

Alisisitiza kuwa mahakama inafahamika kuwa ni zao la katiba na sheria, hivyo ilichokuwa inatakiwa ni kutoa maelekezo kwa kufuata vifungu vya sheria.

Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza alisema hatua hiyo ni sawa na kesi kupelekwa mahakamani halafu mahakama ikatoa amri kuwa kesi hiyo ikasikilizwe kifamilia na kufafanua kuwa hatua hiyo haiwezi kutoa haki kwa anayeshitaki na aliyeshitakiwa kwa kuwa familia itapendelea upande mmoja.

Wakati huohuo na wanaharakati wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), wameibuka na kuipinga vikali hukumu hiyo.

Wanaharakati hao sasa wanajianda kulifikisha suala hilo kwenye mahakama (African court of Justice and Human right) yenye makao makuu mjini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Mkurugenzi wa kituo hicho, Francis Kiwanga alisema maamuzi hayo yanayonyesha mahakama kushindwa kufanya kazi yake ya kutafsiri sheria kama ilivyopewa mamlaka hayo na katiba.

“Ikumbukwe kuwa msingi mkuu wa utawala bora ni kutofautisha majukumu na mamlaka ya mihimili ya nchi ambayo ni Mahakama, Serikali na Bunge, kama mahakama inakiri kutokuwa na mamlaka ya kutoa haki ni chombo gani kingine kinaweza kuwa na mamlaka hiyo?”alihoji Kiwanga na kuongeza;

“Kituo kinaanda jopo la wataalamu wa sheria ili kupeleka suala hili kwenye vyombo vya kimataifa vya utoaji haki,”alisema Kiwanga.
Kiwanga alisema mahakama ndio chombo peke kikatiba kinachotakiwa kutafiri sheria na kutoa maamuzi bila upendeleo wowote.

Sunday, June 6, 2010

KURUHUSU KUTUMIA LUGHA ISIYO KISWAHILI KWENYE KAMPENI NI UBAGUZI MKUBWA TANZANIA

MAJIBU KWA TUME YA UCHAGUZI, TANZANIA, YA MAAMUZI YA KURUHUSU KUTUMIA LUGHA ASILIA ZA JADI KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2010 NCHINI TANZANIA.

Jambo hili la kuruhusu matumizi ya lugha za asili katika kampeni za uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2010 nchini Tanzania, ni kukiuka, kuvunja na kudhihaki Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa sababu kuna Ibara nyingi tu katika Katiba hiyo zinazokataza katakata ubaguzi kama huu.

Ibara hizo ni pamoja na Ibara ya 12, 13, 18, 19, 20, 21. Inashangaza kwamba Jaji Mzima wa Tume ya Uchaguzi Tanzania anafikia hatua ya kutangaza uhalali wa jambo hili ambalo Watanzania wote tunalipigia kelele tangu uhuru wetu tarehe 9/12/1961. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndiye aliyekuwa wa kwanza kukemea na kuhakikisha ukabila unapotea nchini Tanzania katika mambo ya Kiserikali kama haya kwa kukidumisha, kukienzi na kukitumia KISWAHILI na mapema sana kuitangaza lugha hiyo utumiwayo na Watanzania wote kuwa ndio lugha ya TAIFA hili. Kiingereza kikifuata kuwa lugha ya pili ya Kiofisi na kibiashara.

Naunga mkono kwa asilimia mia moja (100%) kwamba jambo hili lipigwe vita hadi kieleweke. Jaji Makungu hana haki ya kuturudisha nyuma Watanzania katika enzi za kabla ya uhuru wetu. Jambo hili ni hatari, halifai, halipaswi hata kufikiriwa licha ya kutekelezwa. Makungu ni adui wa nchi hii. Tafadhali rejea habari iliyo hapa chini ili uelewe juu ya jambo hili kikamilifu.
__________________________________________________________________________



By PIUS RUGONZIBWA, 4th June 2010 "Daily News", Tanzania
>
>
> CANDIDATES will now be allowed to campaign using tribal languages
> during this year's general elections provided they do not offend
> other contestants.
>
> The National Electoral Commission (NEC) Vice- Chairman, Judge Omary
> Makungu, said this during a meeting of stakeholders from various
> political parties in Dar es Salaam yesterday to deliberate on the
> electoral code of conduct.
>
>
> He said that the Commission will consider their views and include
> tribal languages during campaigns in this year's general elections.
>
> "We are going to prepare guidelines on how and when to use tribal
> languages and making sure they are not used to offend others and
> disrupt the peace," he explained.
>
>
> The stakeholders were against the Commission's proposal that only
> Kiswahili should be used simply because it was understood by the
> majority of the population and that interpreters would be used in
> areas where the language is not understood.
>
>
> They stressed that it was important that vernacular or tribal
> languages be used to deliver the right messages to voters,
> particularly those in rural areas and who don't understand
> Kiswahili thoroughly.
>
>
> "Tribal languages are inevitable as experience has shown that many
> people especially in remote areas are not conversant with Kiswahili
> despite the fact that it is the national language," said Mr John
> Mnyika from Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
>
>
> The same sentiments were echoed by National League for Democracy
> (NLD) and CCM whose representatives argued that using interpreters
> would be wastage of time and resources. They also argued that
> number of interpreters was too limited to meet the demand during
> the elections.
>
>
> The meeting also suggested the time for ending campaigns to be
> rescheduled from the current 6:00 pm to at least 8:00 pm, but NEC
> officials said due to different geographical locations, it was
> better that campaigns end at at least 6:30pm.
>
>
> NEC, however, concurred with stakeholders' views that campaigns
> using loud speakers be extended to 8:00 pm instead of 7:00pm at
> present.
> Meanwhile, stakeholders were against the mandatory requirement for
> parties to sign and accept this year's electoral code of conduct
> otherwise they would be barred from taking part in the elections.
>
>
> They also opposed another section providing that any candidate who
> refuses to sign and abide to the code of conduct will automatically
> be disqualified from contesting in the elections.
>
>
> "We must avoid threats if we want to make this law a success. Such
> threats are unconstitutional since every citizen has the right to
> elect and be elected regardless of his or her status," said Mr
> Emanuel Makaidi, TADEA Chairman.
>
>
> The Commission also warned stakeholders against using religious
> places like churches and mosques to conduct campaigns, saying such
> practices might instigate violence.
>
>
> ___________

Saturday, June 5, 2010

WAZIRI MWAKYUSA KATOA KAULI ZA KEBEHI NA BEZO KWA WANAWAKE WA TANZANIA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa alipotoka sana tena sana kwa kauli yake ya kwamba "Suala la kujifungua kwa wanawake kuwa starehe badala ya majonzi" yanayotokana na vifo vya kinamama hapa nchini Tanzania; aliyoitoa tarehe 5 Aprili, 2010 jijini Dar es Salaam, TANZANIA, na kunukuliwa na Gazeti la NIPASHE.

Kwa kweli haiwezi kupita bila kutolewa kauli ya marekebisho na sisi wanawake wenyewe tuliopitia na tunaoendelea kupitia MTULINGA wa kujifungua.

Profesa kwa kuwa ni mwanaume hawezi kupata chembe ya hisia za machungu anayopitia mama anayejifungua. Haijalishi endapo mzazi huyo ataishi au atapoteza maisha. Hivyo Profesa tunamtaka arekebishe kauli yake kwa sababu inaleta hisia za kubeza na kukejeli masaibu ya uchungu yanayotukuta wanawake wakati wa kujifungua.

Tunamhakikishia Profesa Mwakyusa kwamba hakuna starehe yeyote katika zoezi zima la kujifungua na hivyo ni kauli ambayo haikustahili kutolewa na mzungumzaji Kiswahili kama yeye aliyelelewa chini ya uongozi wa Baba wa Taifa. Ikumbukwe kwamba Profesa Mwakyusa alikuwa Daktari binafsi wa Mwalimu Nyerere kwa miaka mingi na hivyo tungetaraji kwamba yeye angekuwa mstari wa mbele katika kutumia misamiati mwafaka katika hotuba zake.

Suala la kujifungua sio suala la kulitafutia lugha ya kibiashara kama hii, kwa sababu linaleta hisia kali sana kwa wanawake waliojifungua na wanaoendelea kujifungua popote pale walipo.

KAULI YA TAMBE HIZZA NI UVUNJAJI WA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

HAYA NI MAJIBU JUU YA HABARI ILIYOTOKA KATIKA GAZETI LA NIPASHE LA TANZANIA LA IJUMAA, MEI 21, 2010, UKURASA WA TATU, ILIYOKUWA NA KICHWA CHA HABARI KISEMACHO "CHADEMA YADAI CCM IMEANZA KUCHEZA RAFU".

Mkurugenzi wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, TAMBWE HIZZA aliyesema "Tunahakikisha kila mwanachama wetu anajiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura ili siku ya uchaguzi apige kura na ambaye hatafanya hivyo hataruhusiwa kupiga kura za maoni ndani ya chama" (cha CCM) ni kauli ya kuivunja ibara ya 5 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa sababu zifuatazo:

1. Haki iliyotajwa ya kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania na ni haki ya hiari. Yawezekana mwananchi au raia hapendi kujiandikisha kupiga kura, hivyo halazimishwi kufanya hivyo, kulingana na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo kuiunganisha na kulazimisha haki ya kupiga kura chamani CCM na haki ya kujiandikisha kupiga kura ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kumnyima haki mwana-CCM katika uhuru wake wa kupiga kura katika kura za maoni.

Hata kama hiyo kanuni iliwekwa katika Katiba au Taratibu na Kanuni za CCM juu ya jambo hilo, chama hicho kinatakiwa kitambue kuwa kanuni au taratibu hiyo inavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, hivyo ifutwe mara moja Kanuni hiyo inayokwenda kinyume na Katiba yetu.

Sababu za au ZUIO la Mwananchi wa nchi hii kupiga kura zimeaorodheshwa katika Ibara ya 5 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Hivyo kigezo kinachosema lazima mpiga kura za Maoni ndani ya CCM awe na Kitambulisho cha kupiga kura sio moja la ZUIO ninalolizungumzia ndani ya Ibara ya 5 (2). Hivyo ni kumvunjia haki yake mwanachama wa CCM ya kupigia kura amtakaye katika kura za maoni katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu Octoba 30, 2010.