Imechangiwa na dar.millionaire@gmail.com
Kanuni ni kama ifuatavyo:
1. Kwa nini unaanzisha blog?
- Unajifurahisha tu kama hobby?
- Unataka kuelimisha jamii
- Unataka kuanzisha libeneke (yaani kampeni dhidi ya tatizo fulani mpaka kieleweke)
- Unataka umaarufu (mfano watu wajue wewe ni VP)
- Unataka pesa (mfano kuvutia wasomaji wengi na kuuza nafasi za matangazo, au kupromoti biashara zako binafsi)
- Yote hapo juu
- Sababu nyingine ..
2. Then ukishaamua malengo ya blog kinachofuata ni kuchagua topic.
3. Katika kudumisha blog kuna technic za kawaida na za kiufundi. Za kawaida ni:
- Post article kwenye blog yako at least mara moja kwa wiki. The more frequent the better.
- Changia mijadala kwenye globu za wengine kwa kutumia ID yako ya kublogia ili mtu kama kapenda mchango wako abofye ID yako kuona blog yako. (Mwl. Mbele anafanya sana hii)
- Anzisha hoja katika blog na forums za wengine na hakikisha unaweka link ya blog yako.
- Tengeneza video isiyozidi dakika 3 itundike kwa Youtube.com kisha ichomoke kwenye blog yako ... weka relevant tags kama tanzania, africa, jina lako, hoja yako, nk. A video will make you look very important like a VP. Baada ta kukamilisha video toa taarifa kwa wanablog kumi walio juu kwamba "Kuna video ya Mzee K anongelea a, b,c,c d..."
Kuna mbinu nyingi zaidi, sema inategemea na malengo ya blog.
No comments:
Post a Comment