From Sara Mrema (machomrema@yahoo.com)
Tarehe: Februari 20, 2009, 7.30am.saa za Afrika Mashariki.
Kwa kweli Bwana Afande AGP Saidi Mwema ana kazi nzito.
Napenda kuwataatharisha kuwa muwe makini zaidi mkiwa barabarani hasa kwenye foleni.Kuna kundi la vijana zaidi ya 30 wanavamia magari wakiwa na mapanga,nondo na visu kwa lengo la kupora chochote ulichonacho na halikadhalika wanauwa ama kujeruhi. Maeneo hatari ni maeneo ya Jangwani- Morogoro Road ,Ocean Road, Seaview, Salender Bridge , Bonde la Kigogo ukitokea
Ilala kuja Magomeni, Daraja la Ubungo karibu na njia panda ya kwenda UDSM na barabara ya Mandela Road ukitokea Tazara kuja Ubungo (NDIPO ALIPOVAMIWA RAFIKI YANGU) His Case. Akiwa kwenye folen majira ya saa mbili
usiku, ghafla lilitokea kundi la vijana kama kumi na mapanga na kuanza kupiga vioo vya gari wakitaka kuvunja, aidha waliongezeka ghafla na wakafunga barabara kama kwa dakika 7 hivi wakiendelea kumshambulia (kwenye gari walikuwa watatu), kumbuka kwenye foleni huwezi kukimbia popote, Mungu aliwasaidia sana kwani milango ya gari ilikuwa imefungwa/locked, na vioo vilikuwa vimefungwa kasoro kimoja kilikuwa wazi nusu. Baada ya mapambano na kelele za kuomba msaada,ndipo msamalia mwema aliyekuwa na silaha aliingilia kati na ndipo alipowatawanya. Kwa mujibu wa Taarifa mbalimbali, haya matukio yamekuwa yakiongezeka sana katika siku za usoni, kwa hilo nawatahadharisha msinunue vitu ovyo kwenye traffic light, vioo msishushe ovyo na lock za milango ya magari mfunge, muwe makini.Ujambazi huu unafanyika kila siku sehemu tofauti kuanzia saa 12 jioni kuendelea. Namshukuru Mungu hakuna aliyeumizwa sana , japo walifanikiwa kupata baadhi ya vitu ikiwemo simu ya mwenye gari. Natambua unaweza kuona kama sinema,ila haya ndio yanayotokea katika jiji la Dar kwenye foleni za magari.Mwatawala, Zainab M.
P O Box 453
Morogoro, Tanzania
East Africa
Tel. 255 023 260 3583
Cell: 202 427 4413
5167 Fulton Str. NW
Washington, DC., 20016
USA
Many thanks for the exciting blog! I really enjoyed reading it. Great Job,Keep it up..
ReplyDeletebest mhe leasing companies in qatar