Saturday, February 14, 2009

UTANI USIOFAA - A JOKE IN VERY BAD TASTE

JAPO ujumbe huu unatarajiwa kuonyesha baadhi ya kejeli ya wananchi kwa mambo yanavyokwenda nchini Tanzania katika nyanja tofauti, lakini kuingiza sentensi ya mwisho ni kukebehi vifo vya kweli vitokeavyo hivi sasa nchini tokana na imani za kishirikina.

Jambo hili si la utani na wenye familia zenye walemavu kama hao wamo katika jakamoyo kubwa na tunastahili kusaidiana nao kutafuta ufumbuzi wa kutatua tatizo la mauwaji ya zeruzeru na sio kuwakebehi namna hii.
IWEJE SIKU IDHANIWAYO NI YA WAPENDANAO KUINGIZA JAMBO HILI! Hili si jambo la mwenye kiranga haliliwi. Hawakuomba kuwa hivi!

Here's a message circulating in the country since yesterday via SMS

Please pick it up and forwar to at least 10 people. WHY? Is this a chain Letter?


Katika siku ya wapendanao... Nakuombea furaha yako iongezeka kama bei ya petroli; Mashaka yapungue kama kura za CCM 2010; Umaarufu wako uongezeke kama Orijino Komedi; Hekima zako zizagae kama bidhaa za Mchina; Uwepo wako kila mahali uwe wa thamani kama kiungo cha albino. HAVE A WONDERFUL VALENTINE DAY.

No comments:

Post a Comment