Thursday, February 19, 2009

HIZI NDIZO ELIMU ZA VIONGOZI WETU TANZANIA!

WANDUGU, nyuso zetu tutaziweka wapi mbele ya Waafrika wenzetu (achilia mbali duniani) kama hali ndio hii?

Fwd: [UDASA] Re: HIZI NDIO ELIMU ZA VIONGOZI WAKO] Imechangiwa na Geoffrey Gitagia.
HIZI NDIO ELIMU ZA VIONGOZI WAKO Naomba ieleweke kuwa kuna makundi mawili hapa tunayoyaongelea: La kwanzani kundi la akina Chrisant Majiyatanga Mzindakaya, Jakaya Kikwete , Amani Abeid Karume, Rwakatare n.k. Hawa wana shahada za heshima tu (honoris causa) siyo za kusomea! Chuo chochote kinaweza mtunukia mtu shahada hiyo ya heshima kwa kutambua mchango wake katika jambo fulani. Siku za nyuma hata baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Spika Adam Sapi Mkwawa, Salim Ahmed Salim, Kenneth Kaunda na Milton Obote walipewa heshima hiyo na vyuo mbalimbali duniani.

Kundi lenye matatizo ni lile lenye shahada feki na linadai kuzisomea shahada hizo! Kundi hili ni hatari sana maana linaharibu kabisa heshima, sifa na viwango vya elimu nchini. Wafuatao wana vyeti feki vinavyoitia aibu Serikali na nchi ya Tanzania kwa ujumla:

(1) Salmin Amour - Ph.D yake ni feki, ya kisiasa. Aliipata UjerumaniMashariki enzi hizo kwa miezi mitatu tu huku akiwa na cheti cha form fourtu!

(2) Pius Ng'wandu - Ph.D yake ni feki. Chuo anachodai kusoma cha Stanford,Marekani hakina kumbukumbu zake. Aliosoma nao huko Marekani, akina Prof.Baregu, wanajua kuwa ana Masters tu!

(3) Mary Nagu - Ph.D yaje ni ya kununua kwenye mtandao.

(4) Emmanuel Nchimbi - Ph.D yake ya uchumi ni ya kununua. Hana uelewa wowote wa economics kichwani mwake.

(5) Makongoro Mahanga - Ph..D yake ya ugavi ni ya kununua kama Nchimbi.

(6) Didas Masaburi - Ph.D yake ilinunuliwa pamoja na ya kaka yake Makongoro.

(7) Norman Sigallah - Ph.D yake ni ya kununua kwenye mtandao.

(8) Mafwenga - Ph.D yake sawa na ya Sigallah

(9) Nangale - Ph.D yake ni kutoka chuo kimoja bomu cha chini ya viwango,London .

(10) Mathayo David - Ph.D ya kujipachika.

(11) Mutamwega - Ph.D yake ni feki, ya kununua. Mhusika hawezi kuandikahata sentensi moja sahihi ya Kiingereza.

(12) William Lukuvi - Masters yake ni feki. Kaipata akiwa na sifa za elimu yadarasa la saba na cheti cha ualimu, class C.

(13) Samuel Chitalilo - Vyeti vyake vya elimu ya juu toka Uganda vyote nifeki. Ana kesi ya kujibu mahakamani!

Nimepata taarifa mbalimbali kuhusu vyeti vyaWabunge wafuatao:
(1) Sigonda. Namfahamu sana Mbunge Sigonda. Ni mtu wa Usalama wa Taifa aliyeishia darasa la nane. Leo naambiwa ni Dk.!
(2) Kapteni John Komba,
(3) Omari Mzeru na
(4) Savelina Mwijage.Nazifanyia kazi. Nitazianika hapa muda muafaka!Ijabu Ijabu kanipa hamasa sana juu ya suala hili. Wote aliowaeleza kweliwana vyeti feki na hata ukiongea nao, ni vihiyo vihiyo wa kutupwa!

Naomba niongeze majina mengine kwenye listi la
(5) Mhe. Diodorus Buberwa Kamala,Mbunge wa Mkenge na Waziri wa A. Mashariki. Huyu bwana kasoma Mzumbe kama Nchimbi ambako mtandao wa vyeti feki ulianzia na
(6) Mkuu wa Chuo hicho Bw.Moses Daudi Mhonwa Warioba. Ph.D yake ni feki, ni ya kununua kama hizo za wenzake aliowataja Ijabu. Hata kwenye Bunge la A. Mashariki tunaambiwa anapwaya ile mbaya.
(7) Naibu wake, Mohamed Aboud, yeye ndo balaa maana ni form four failure na CVyake inasema uongo kuwa ana diploma ya Uingereza! Wote ni Ze Komedi mbele ya Wakenya, Waganda, Warwanda na Warundi!
(8) Yupo huyu mama wa Kibaha, Zainab Gama. Anajiita Dk. wakati ana diploma ya Radiology tu!
(9) Kuhusu Mbunge Savelina Mwijage (Viti Maalum, Kagera), huyu ana matatizomakubwa maana anatumia jina la marehemu. Taarifa zote zilitoka gazetini,lakini analindwa. Hawezi hata kuandika jina lake, lakini ni Mbunge.Anayebisha aje na ushahidi maana huyu mama namfahamu miaka mingi akiwamfanyakazi wa ndani wa Mhindi Bukoba. Hebu tupe dataz Ijabu na wana JFwengine.

Capt. Komba yeye ni msanii na mwizi asiyestahili kujadiliwa hapa maana anawaibia hata wasanii wenzake dani ya Tanzania One Theatre (TOT). Mzeru wa Morogoro yeye ni mafix moja kwa moja. Hana udaktari wowote! Alijipachika udaktari kuombea ubunge na unaibu waziri kwa Jakaya Kikwete!

(10) Agustino Lyatonga Mrema - Pacific Western University , a diploma mill. Yeye alipoenda kuchukua hiyo "degree" alikwenda na matarumbeta kibao, vifijo nanderemo.

(11) Mustafa Mkullo - Almeda University , a diploma mill. Kule youngafrican.comnakumbuka ilisema eti chuo chake kiliwahi kutoa associate degree kwa mbwa anayeitwa "Wally" mali ya mwandishi mmoja wa habari huko Marekani (In 2004 the CBS affiliate in Albany , New York , ran a report on Almeda that featured Peter Brancato, who had filled out an application for an associate degree on behalf of his dog, Wally. Part of the "life experience" listed on the application was "Plays with the kids every day... teaches them to interact better with each other ... Teaches themresponsibilities like feeding the dog." Almeda granted Wally anassociate's degree in childhood development with a course list including European culture, college algebra, American history, and public speaking.In reply, Almeda claims Brancato perjured himself by creating a false identity using a fabricated name and date of birth. They write, "He completed an application that included a background of the following: Eight-years tutoring pre-K children,curriculum design and development, teaching coping skills, and volunteer coaching."" Almeda University - Wikipedia, the free encyclopedia.

(12) Kama sijakosea waheshimiwa wengi sana wana degrees kutoka chuo cha Washington International -I think even Sofia Simba anayo ya huko.

Yona Fares Maro Master of Science in Computer Science and Information Systems (MS) University of Michigan-FlintThank You

Regards Geoffrey Gitagia: Tel-0721419305

No comments:

Post a Comment