Tuesday, February 3, 2009

WANAFUNZI CHUO KIKUU GEORGETOWN WASUBIRI BASI KWA FOLENI

Wandugu,
Leo hii katika pilika za shule yangu huku, nimekutana na foleni ndeeefu huko Du Pont Circle. Nikajiuliza kulikoni? Kumbe nikapata jibu mara baada ya kuwasili basi la Chuo Kikuu cha Georgetown! Walikuwa wanafunzi wanasubiri basi la shule.

Liliposimama tu, wanafunzi wale wakaingia ndani ya basi kistaarabu sana bila bughudha hadi wakaisha. Japo nipo American University tangu Agosti 2008, sijawahi kuona wanafunzi wa American University wakisubiri basi lao kwa foleni kama hawa vijana wanafunzi wa Georgetown University. Kwa kweli nimewasifu sana moyoni kwa utaratibu wao huu mzuri wa kujipanga wakisubiri usafiri kwenda chuoni kwao.

Je, huu si mfano mzuri sana wa kuigwa na wanafunzi wa Vyuo Vikuu Vyetu pia? Heko wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Georgetown, Washington DC, USA !

No comments:

Post a Comment