Sunday, February 8, 2009

SOMO LA AFYA BORA NA. 2

Kutoka kwa Dr. Wilbert Bunini Manyilizu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Tanzania; Januari 18, 2009.


MWENDELEZO WA ARTICLE 1

Kuna njia nyingine pia ya kujichunguza kuona kama uzito uliozidi unamhatarisha mtu kupata magonjwa yanayoambatana na kitambi.

Njia hii ina vigezo vitatu vya kuangalia, hivi ni pamoja na BMI hapo juu, mzunguko wa kiuno na tatu vigezo vya hatari vinavyoambatana na kitambi.

Kimsingi BMI hupima uzito wa mhusika unavyohusiana na urefu wake na kutoa picha ya mafuta mwilini kwa jumla wakati huo mzunguko wa kiuno hupima mafuta ya tumbo. Hivi viwili vikiunganishwa hutoa hatari ya nyongeza ya kupata maradhi na vifo vinavyoambatana na kitambi. Msomaji anaweza kuzungusha tepu yenye vipimo kuzunguka kiuno, hii hutoa picha ya mafuta ya tumbo ambayo pia ni kigezo cha hatari cha kupata magonjwa ya moyo, kisukari kiharusi na mengineyo. Hatari huongezeka kadri kiuno kinavyoongezeka zaidi ya inchi 40 (sentimita 102) kwa wanaume na inchi 35 (sentimita

89) kwa wanawake.

Vigezo vingine vya hatari mbali na vile vya BMI na mzunguko wa kiuno ni kama ifuatavyo: -

Kuwa na shinikizo la damu (BP ya juu)

Kuwa na kolestero mbaya nyingi kwenye damu (LDL)

Kuwa na kolestero nzuri kidogo kwenye damu (HDL)

Kuwa na glukosi (sukari) nyingi kuliko kawaida kwenye

damu Kuzaliwa kwenye ukoo wenye asili ya magonjwa ya moyo

Kutokufanya mazoezi ya viungo

Uvutaji wa tumbaku (sigara)

Ushauri

Kawaida kitambi hupenda mapumziko na kuepa shughuli na kuhangaika. Wakati huo huo mapumziko hutunza kitambi kiendelee

kustawi. Kama hili linamtokea msomaji basi ni bora kuchukua tahadhari mapema. Kwa yule atakayegundua kuwa ana kitambi (BMI kuanzia 30 au zaidi) au mwenye uzito uliozidi (BMI kuanzia 25 hadi 29.9) na ana vigezo viwili au zaidi vya hatari anashauriwa apunguze uzito. Hata kama ni moja ya kumi

ya uzito itapunguzwa itasaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yanayoambatana na kitambi.Wagonjwa wenye uzito kuliko kawaida, lakini hawana viwango vya juu vya kiuno na wana vigezo chini ya viwili vya hatari, wanashauriwa wasiruhusu kuongeza uzito zaidi ya ule walionao.Daktari atashauri kama mgonjwa apunguze uzito. Watu walio na uzito uliozidi na wale wenye vitambi wana hatari ya kupata magonjwa yaliyotajwa na pia kansa kuliko wale wenye uzito wa kawaida.Kuna vigezo vingi na mbinu nyingi ambazo zinaweza kutumika au kudhibitiwa na kuondoa hatari ya kupata magonjwa haya hata kama mtu anatoka katika ukoo wenye magonjwa hayo.Kwa kubadili mtindo wa maisha, ulaji na unywaji.

Kufanya kazi kwa bidii, kuacha uvivu na kupunguza mapumziko.Kuacha kula ovyo ovyo bila utaratibu. Epuka vyakula vya mafuta na punguza kula nyama au nyama za mafuta. Kula kwa kiasi si kwa kuongozwa na tamaa au hamu.Kuacha uvutataji sigara (tumbaku), sigara ni moja ya vigezo vya hatari viletavyo vifo vya ghafla. Hatari ya kupata ugonjwa ni mara mbili zaidi kuliko wasiovuta. Wavuta sigara wenye ugonjwa wa moyo wana hatari ya kufa kuliko wenye ugonjwa huo wasiovuta. Kwa kuacha uvutaji hatari hupungua mara moja.Kufanya mazoezi ya mwili na viungo, mazoezi ya mara kwa

mara yasiyo ya nguvu, hata kutengeneza bustani jioni yanatosha kurekebisha kolestero, shinikizo la damu, na kuondoa hatari ya magonjwa hatari. Muone mtaalamu wa mazoezi kukuelekeza mazoezi yapi yafaa zaidi kwa afya.

Punguza kitambi.

Dhibiti kisukari kwani huongeza hatari ya kupata magonjwa

mengine, shinikizo la damu kwa kuzingatia ushauri wa

tabibu.

Dhibiti msongo na hasira.

Epuka unywaji pombe.

Kunywa maji mengi kila siku

Kushirikiana na wenzi katika mambo mbalimbali hata katika

kutatua matatizo

Epuka vyakula vya chumvi nyingi na pia kuongeza chumvi

mezani.

Epuka vyakula vya kukaangwa Chagua mafuta yenye hatari kidogo katika vyakula vyako

hasa yale yatokanayo na mimea.

Kula zaidi vyakula vya asili, mboga mboga, matunda, na

nafaka kiasi, kwani wengine wamenenepa si kwa kula

vyakula vya mafuta bali kwa sababu wanakula kiasi

kikubwa cha wanga.

Aina kuu za kolestero

Kolestero siyo mafuta. Isipokuwa ni kemikali inayonata inayopatikana katika vyakula vyenye asili ya wanyama; kama nyama, aina za kuku, vyakula vya baharini, kiini cha yai, maziwa ya krimu. Mwanadamu hahitaji kutumia kolestero sababu miili inaweza kutengeneza kolestero zake kwa mahitaji ya ngozi za chembe chembe (cell membrane) na pia kwa ajili ya homoni. Kupata kolestero isiyohitajika ni kuleta magonjwa ya mishipa ya damu na magonjwa ya moyo, kiharusi (stroke), kisukari, kansa na mengineyo.

LDL (Low Density Lipoprotein) - Aina hii ya kolestero ni mbaya kwani huleta magonjwa ya moyo. Kwani aina hii ndiyo inayoleta kulundikana kwa kemikali hii inayonata kwenye mishipa ya damu. Kolestero husafirishwa kwenye damu kama lipoprotini bila kuchanganyika na damu yenyewe kama ilivyo

kwa maji na mafuta yanapokuwa kwenye chombo. Kulundikana huku ndiko husababisha mishipa kuanza kuziba na kuleta matatizo ya moyo. Hali akuwa mbaya zaidi kama mhusika anakuwa tayari na magonjwa kama ya moyo, shinikizo la damu, kisukari na mengineyo yanayoambatana na unene.

HDL (High Density Lipoprotein)

Aina hii husaidia kuepusha magonjwa ya moyo. Aina hii huwa na nafuu kidogo ikilinganishwa na ile iliyotajwa hapo juu kwani hii huchukuliwa na kupelekwa kwenye ini na kubadilishwa kuwa kitu kingine na kutolewa nje, njia ambayo huifanya isiwe na athari kwenye mishipa ya damu. Lakini pia aina hii inapotumiwa kwa kiasi kikubwa isivyokawaida ini hushindwa kuiondoa yote na hivyo kulundikwa kwenye mishipa na kusababisha madhara yale yale kama kolestero ile ya hatari.

Mafuta mazuri kiasi kwa afya na salama kwa moyo

Mafuta ambayo huwa yako katika hali ya kimiminika katika joto la kawaida (room temperature) huitwa Unsaturated fats. Lakini mafuta haya yaweza kutiwa haidrojeni kidogo katika kuyasindika yakae muda mrefu, kwa kuyatia haidrojeni basi huganda na kuyafanya yaingie kwenye kundi la mafuta ya hatari (trans fat). Umbo la kikemia la mafuta haya hupatikana zaidi kwenye vyakula vinavyotokana na mimea, pia hupatikana kwenye samaki wanaokula mimea midogo midogo mtoni, ziwani au baharini. Aina nyingine katika kundi hili la mafuta ni ya Omega 3 (omega 3 fatty acids). Utafiti unaonesha kuwa mafuta haya yana faida, kwa mfano, hupunguza vifo vya ghafla vinavyotokana na moyo, kwa sababu husaidia kuondoa ugumu au ukakamavu wa mishipa

ya damu na pia huzuia damu kuganda isivyohitajika. Mafuta mengine katika kundi hili ni ya (polyunsaturated fats) na jingine ni lile la (monounsaturated fats). Aina hizi hapa juu hupunguza aina hatari (mbaya) ya kolestero (LDL).

No comments:

Post a Comment