Wednesday, February 4, 2009

VILEMBWE VYA WATUMWA WANAPETA MAREKANI

Jumanne, tarehe 3 Februari, 2009 Gazeti dada la Washingtonpost, EXPRESS la Washington DC, USA, limeripoti kuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika Bwana Eric Holder amethibitishwa na Bunge (Senate) la nchi hiyo kushika wadhifa huo.

Bwana huyu anakuwa ni mtu wa tatu kufungua njia ya wenye asili ya Kiafrika kupata vyeo vya juu nchini Marekani katika nafasi za kuchaguliwa au kuidhinishwa na Bunge.

Wa kwanza kufungua njia hiyo ni Rais Barack Hussein Obama aliyechaguliwa na Wamarekani na kuapishwa kuwa rais wa 44 wa nchi hiyo tarehe 20 January, 2009 na mwingine ni Mwenyekiti wa Kwanza wa Chama cha Republican aliyechaguliwa wiki iliyopita.

Hivyo kwa Bwana Ralph Nicoletti (18), aliyeandikwa habari zake katika gazeti hilo hilo, kwamba atarajie miaka 12 ya jela kwa kuzusha valangati siku ya Uchaguzi Novemba, 4, 2008 hadi kusababisha mtu mmoja kupata kiharusi na kutojitambua (comma) kwa sababu ya chuki yake ya kuchaguliwa Kilembwe cha Watumwa kazi kwake. Jamani, kwa kupeta huku kwa vilembwe vya watumwa, yeye si ALIYE TU?

No comments:

Post a Comment