Wednesday, February 4, 2009

STEMPU YA $0.94 kwa SHILINGI 800/= za TANZANIA

Leo hii tarehe 4 Februari, 2009 nimetoka posta iliyo jirani yangu kuposti barua ya uzito wa chini kabisa kutoka Hapa ninapoishi "The Palisades", Washington DC hadi kwenda Morogoro, Tanzania, Afrika Mashariki. Nikauliza bei ya stempu nikaambiwa ni senti 94 (huku inaandikwa hivi $0.94) yaani dola sifuri, senti tisini na nne. Juzi nimepokea barua kutoka Dar es Salaam, Tanzania iliyowekewa stempu ya Tshs.800/=. Kwa maana hiyo, kwa kulinganisha gharama hizo mbili ndio nasema hivi; fedha za Tanzania Tshs.800/= ndio sawa na hiyo senti tisini na nne ya Marekani; angalau kwa upande wa kuposti barua.

Kwa upande wa misosi (vyakula), ndio ukiangalia dola inavyonunua vitu huku ukilinganisha na fedha za kwetu, hutanunua kitu. Maana kwa kitu cha kawaida kabisa huku, mkate; mmoja wa bofulo unanunuliwa kwa bei ya hapa Washington DC, ni dola mbili na senti tisini na tisa ($2.99). Kwa ulinganifu wa fedha zetu ambazo kwa sasa kwa wastani ni kama dola moja kwa shilingi elfu moja ($1 = 1,000/=), basi mkate mmoja hapa Washington DC ni sawa na fedha za Tanzania Tshs.2,990 (elfu mbili mia tisa tisini). Hivyo ukilinganisha bei za vitu huku na huko nyumbani, hutanunua kitu. Vitu hasa vyakula ni ghaaaaaali mno. Kwa sasa nafahamu bei ya mkate wa kawaida kabisa ni shilingi mia tano (Tshs.500/=).

No comments:

Post a Comment