Wandugu,
Huku katika taifa la Marekani (USA) kazi za majaji, Walimu wa Vyuo Vikuu vyote ni kazi ya Maisha. Maana yake haina mwaka wa Kustaafu kwa Mujibu wa Sheria. Hivyo kwa vyeo hivyo, mtu akishakipata, ni pale tu Mungu atakapomuamulia ukomo wa uhai wake (au afya yake ikiathirika vibaya).
Wenzetu huku mwalimu na jaji kadri unavyozeeka ndio kadri unavyokuwa gwiji, hivyo hakuna suala kustaafu endapo una afya njema na unaweza kuendelea na kazi yako. Nimeona jambo hili nzuri sana kwa nchi zetu za Kiafrika. Kwa bahati mbaya tumeamua kujiwekea ukomo wa umri wa kufanya kazi hadi miaka 60, 70 na wengine 75. Wenzetu hawana hayo. Ili mradi ari unayo, uwezo unao, basi unaendelea kufanya kazi hadi utakaposema mwenyewe kuwa nimechoka nastaafu.
Kwa maana hiyo, wenzetu wanawatumia wataalam wao kwa uwezo wao wote kwa umri wao wote. Kwa nini sisi tunajiwekea ukomo kwenye vipaji vya kitaalam kama hivi? Naamini hata madaktari huku ni maisha japo kwa wao wanafanya kazi binafsi. Ingekuwa ni waajiriwa serikalini au mashirika, nao pia wangeingia katika mkumbo huo huo kuwa wangestaafu kutokana na kuchoka wenyewe sio KWA MUJIBU WA SHERIA YA UKOMO WA MIAKA.
No comments:
Post a Comment