Tuesday, August 21, 2012

MAONI YA KATIBA KWA TUME YA KATIBA NA. 2


MAONI YA  KATIBA NA. MBILI – 21/8/2012
SHERIA  YA MAREKEBISHO YA KATIBA NA. 8 YA 2011. 
Kifungu cha 17 (4) naomba kiongezwe kipengele cha 17 (4) (o) nacho kiongeze Ripoti ya Sensa ya Watu na Makazi Tanzania ya  Mwaka 2002 iliyogundua kwamba Watanzania tuko Wanawake asilimia 51 na wanaume asilimia 49.  Jambo hili linawezekana chini ya kifungu cha 17 (4) (n) cha Sheria hiyo. 
a.    Kwamba katika kila Mkutano wa Kukusanya maoni ya Wananchi, watazingatia idadi ya wahudhuriaji na kurekodi wanawake asilimia ngapi na wanaume asilimia ngapi.
b.   Kwamba katika kila Mkutano wa Kukusanya Maoni ya Wananchi, asilimia ngapi ya wanawake waliohudhuria wameshiriki kutoa maoni na asililimia ngapi ya wanaume wamefanya hivyo.
c.    “The Majority of votes” kama ilivyoandikwa katika Kifungu cha 36 (1) cha Sheria hiyo juu ya “Referendum results” itatilia maanani kwamba katika hizo majority votes endapo itatafsiriwa kuwa ni wanawake wangapi walipiga kura na wanaume wangapi.  Ili ipatikane “majority” itakayothibitisha kwamba pande zote mbili za jinsi zilishiriki kikamilifu katika kupiga kura hiyo ya Maoni na kweli hiyo “Majority Vote” imewahusu wote au la.   Kinyume chake haitastahili kuitwa Majority Vote. 
d.   Mifano ya utaratibu nilioulezea ukifuatwa katika kila kipengele cha Mchakato wa Kuandika Katiba Mpya, kinachotakiwa kuthibitisha idadi ya asilimia ya watu, Tume itakuwa imetenda haki ya kuthibitisha jambo hilo.   Kinyume chake haitakuwa sahihi kusema wamepata majority vote kiasi gani kama jambo hili halitazingatiwa.  Tume haijachelewa kutekeleza hili. 


No comments:

Post a Comment