Monday, April 6, 2009

SERIKALI YA SHIRIKISHO LA MAREKANI (USA) HUTUMIA DOLA BILIONI MOJA KWA SAA

Wandugu, hiyo mpya nimeipata leo hii Aprili 6, 2009 hapa Washington DC katika gazeti la "Washington Examiner" litokalo kila siku za kazi mjini hapa.

Ni ajabu na kweli. Mhariri analalamika kwamba Rais Obama anatoa mpya kuliko wenzie wote waliopita katika matumizi ya bajeti ya Serikali. Gazeti linasema kwamba Bunge limepitisha matumizi ya mwaka 2010 ya Dola Trilioni 3.6; katika mwaka wake wa kwanza na kwamba matumizi haya yataiingiza serikali ya Marekani katika deni la Dola nusu Trilioni kila mwaka kwa miaka kumi ijayo.

Kutokana na mahesabu ya Mhariri huyo wa gazeti hili, hata kabla ya bajeti hiyo kupitishwa, Bunge la nchi hiyo tayari lilishapitisha matumizi ya zaidi ya Dola Trilioni 1.2 ($1.2 trilioni) kwa siku. Hivyo, gharama hiyo ni sawa na matumizi ya Dola bilioni 24 ($24.0) kwa siku. Na hapo ndipo alipopata hiyo hesabu ya matumizi ya Dola Bilioni moja ($1.0) kwa saa tangu Bunge la 111 lilipoanza mwezi Januari, 2009.

Jamani tusichanganye mambo, hapa inazungumziwa bajeti ya serikali ya Shirikisho la Marekani tu. Sio bajeti zilizo nje ya matumizi ya Shirikisho hili. Hivyo hiyo yote ni fedha kwa ajili ya matumizi ya kuendesha Serikali ya Shirikisho la Serikali ya Marekani (USA) yenye majimbo 50 na himaya tegemezi (makoloni - territories) zingine nne ambazo ni Puerto Rico, Guam, American Samoa, Virgin Islands na Makao Makuu ya Serikali ya Shirikisho, yaani Washington DC (District of Columbia).

Kufuatana na katiba yao, hizi himaya tegemezi pamoja na Washington DC zina wawakilishi Bungeni, lakini wawakilishi hao hawapigi kura. Wao ni wasikilizaji tu.

Nilipomuuliza mwalimu Jeffrey Lubbers, profesa wa Sheria za Uongozi (Administrative Law) katika Chuo kikuu cha America (American University) kuwa imekuwaje leo hii katika karne ya 21 nchi ya Marekeni ina himaya tegemezi(makoloni) kama hizi (territories), akanijibu kwamba, hawawalazimishi wananchi wa nchi hizi waendelee kuwa wanatawaliwa na Marekani. Eti lakini kila wapatapo fursa, wananchi hao hukataa kabisa mchakato wowote ule wa kujitawala wenyewe. Kwa maneno mengine, kwao wao, wanajiona kwamba kuwa na sifa ya kutawaliwa na nchi ya USA, wamefika.

No comments:

Post a Comment