Monday, April 20, 2009

MIAKA 15 YA DEMKRASIA YA WENGI AFRIKA YA KUSINI

Leo nimehudhuria Mkutano uliojadili Domokrasia ya watu wengi huko nchini South Africa katika Chuo Kikuu cha Howard (Howard School of Law) kilichopo 2900 Van Ness Str. NW, Washington DC 20001.

Katika Mkutano huo, Profesa Penelope Andrews wa Chuo Kikuu cha Valparaiso, kilichopo jimboni Indiana, USA; aliyeandika kitabu kuhusu mchakato mzima wa Kuandika Katiba mpya ya Kidemokrasia ya Afrika ya Kusini (Post-Apartheid Constitution: Perspectives on South Africa Basic Law); amesema mwaka 1994 wakati wa kuandikwa Katiba Mpya, Afrika Kusini kulikuwa na Majaji 222 walioteuliwa kiholela na Waziri Mkuu. Profesa huyu aliyezaliwa, kukulia na kusomea Afrika Kusini amesema kati ya hao, kulikuwa na wawili weusi, wawili wasiofahamika rangi (coloured?) na waliobaki 218 walikuwa Weupe. Ni katika mazingira ya waheshimiwa hao, ambapo nchi hiyo ilitakiwa kuandika katiba mpya na kushughulikia Kesi za Mahakamani katika mtazamo mpya usiokuwa wa kibaguzi, chini ya Katiba ya Mpito.

Majaji hao kwa mara ya kwanza katika uzoefu wao wa kazi walitakiwa kufuata sheria za haki katika kutoa maamuzi yake, uwazi na ukweli, uwajibikaji, kutumikia dhamira zao (commitment) na kufuata misingi ya Katiba inayokubalika, badala ya kufurahisha mhimili wa utawala, kazi waliokuwa wakifanya huko nyuma.

Nae Balozi wa Afrika Kusini nchini Marekani Mheshimiwa Bwana Welile Nhlapo amekumbusha kwamba waheshimiwa wabunge wa Bunge la Makaburu (Apartheid) la wakati huo wa mwaka 199o ndio hilo hilo lililotakiwa lijitungie sheria lenyewe za KUJIENGUA katika uso wa mihimili ya dola la Afrika Kusini (legislate itself out of existence).

Bwana Welile amesema Mchakato wa nchi yake wa kuleta demokrasia ya watu wengi katika kuandika katiba yake umeigwa pia na Nothern Ireland, Iraq, Burundi, East Timor, Zimbabwe na Sudan.

Nami nikaona kwamba hiki ni kitendo cha kishujaa ambacho Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania hakiko tayari kufanya ili kujisababishia kifo chake chenyewe kwa kuachia demokrasi ya watu wengi kuamua kuhusu hatima ya Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar; Kwa kuandika upya Katiba Shirikishi kama ilivyoandikwa Afrika ya Kusini; ili ijulikane walio wengi wanaamua aina ipi ya serikali ifuatwe na nchi zetu: yaani kati ya zile namna tatu za serikali kama inavyojadiliwa na wananchi kwamba:

1. Iwe serikali moja
2. Ziwe Serikali Mbili kama zilivyo sasa na migogoro yake kibaao inayozidi kunyekenya, au
3. Iwe nchi ya Shirikisho la Serikali Tatu.

No comments:

Post a Comment