Monday, April 27, 2009

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA WASHINGTON MASHINDANONI

Habari hii imetoka kwenye Gazeti la Washington DC "The Examiner" la tarehe 27 Aprili, 2009 ukurasa wa 6, likiwa na habari za Mbio Ndefu kama ifuatavyo:

Mstahiki Meya wa Jiji la Washington DC, ambayo ni Makao Makuu ya Serikali ya Marekani (USA) Bw. Adrian Fenty ameonyesha tena umahiri wake katika mbio ndefu kwa kuisaidia timu yake ya American Odyssey Run Adventure kupata ushindi wa pili katika mbio hizo. Timu hii hukimbia ili kufanya harambee ya kwa ajili ya "The Wellness Community of Greater Washington DC".

Fenty alikuwa ni mmoja wa wakimbiaji 1,300 waliojitokeza kushiriki katika mbio hizo za "relay" iliyofanyika Ijumaa Aprili 25, 2009 kuanzia Gettysburg, jimboni Pennsylvania, kupitia jimbo la Maryland and kumalizikia Jumamosi katika Makumbusho ya Rais Washington. Meya Fenty hakupata shida kukimbia dakika za mwisho za mbio hizi, katika mbio hizo za zaidi ya saa 24. Mstahiki Meya Fenty alisema "nilipotea katika ngwe ya mwanzoni. Nimefurahi kwamba tunamalizia ngwe ya mwisho mchana kweupe"

No comments:

Post a Comment