Tuesday, April 28, 2009

KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA MAFUA YA NGURUWE

Tahadhari za maambukizi ya ugonjwa wa "Swine Flu" kama zilivyochapichwa ukurasa wa tano (5) wa gazeti la Washington, DC la "The Examiner" la Jumanne, tarehe 28 Aprili, 2009.

1. Ukijisikia unaumwa, usiende kazini wala wanao wasiende shule.
2. Osha mikono yako mara kwa mara kuliko zamani na tumia sabuni zenye kemikali za kuulia wadudu.
3. Funika mdomo wako unapokohoa au unapopiga chafya
4. Toa taarifa mapema kwa Waganga namna unavyojisikia ili nao wachukue tahadhari

NAMNA YA KUTAMBUA UGONJWA HUO
1. Kupata homa
2. Kukohoa
3. Kuugua Koo linalokwaruza
4. Kuziba pua
5. Kububujikwa na mafua puani.

Dr. Frank Calia wa Chuo Kikuu cha Maryland amesema ugonjwa huu huchukua kati ya siku moja hadi siku tatu kumpata binadamu. Ndio maana anaamini kwamba ni wale tu waliosafiri hivi karibuni nchini Marekani kuelekea kwenye nchi zenye ugonjwa huo ndio waliomo katika hatari ya kuuambukiza.

No comments:

Post a Comment