Sunday, July 4, 2010

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE WA TANZANIA ADANGANYWA TENA

ON 3 July, 2010, Mwita Chacha wrote:
> JK adanganywa tena, AZINDUA BWAWA WAKATI KESI IKO MAHAKAMANI Send to a
> friend
> Saturday, 03 July 2010 06:18
>
>
> Rais Jakaya Kikwete akifungua bomba la
> maji kushiria kuzinduliwa rasmi kwa mradi wa maji wa Mugumu- Serengeti,
> katika wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara jana, uzinduzi huo ulifanyika
> katika bwawa la Manchira. katikati ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
> Prof Mark Mwandosya Anthony Mayunga, Serengeti
>
> RAIS Jakaya Kikwete amezindua mradi wa Bwawa la Manchira lililoko wilayani
> Serengeti wakati tayari wananchi wamekwishafungua kesi Mahakama
> Kuu ya Mwanza wakidai fidia.
>
> Kesi hiyo iliyofunguliwa ni matokeo ya viongozi wa serikali wilayani hapa kuhusika kuwalipa fidia watu wasiohusika na kuwaacha walengwa waliofanyiwa tathmini.
>
> Kesi hiyo ya madai namba 21/2009 ilifunguliwa katika Mahakama Kuu ya Mwanza
> kitengo cha ardhi chini ya Jaji Nyangarika inahusisha wananchi 77 ambao
> wanadai kiasi cha Sh2 bilioni.
>
> Mmoja wa wawakilishi wa wananchi hao, Jackson Mwita aliwaambia waandishi wa habari wakati wakimsubiri Rais Kikwete bwawani hapo kuwa kutokana na fedha walizotakiwa kuwalipa wahanga wa mradi huo zililipa watu wasiokuwa na maeneo huku uongozi wa
> serikali ukiwapuuza walalamikaji.
>
> Alisema kuwa wanashangaa mradi huo kuzinduliwa kwa mbwembwe wakati tayari Halmashauri imefikishwa mahakamani na wameitwa mara tatu bila kuhudhuria mahakamani.
>
> “Tulipanga kumfikishia Rais ujumbe kwa njia ya mabango, ajue kuwa kadanganywa
> maana eneo lina mgogoro, lakini tumetishwa maana leo anafungua kesho akasikia amri tofauti atabaki kujiuliza kwa kuwa wasaidizi wake si wa kweli,”alisema Mwita.
>
> Hata hivyo, wananchi hao baada ya kutishwa kupitia wenyeviti wa vitongoji
> ambao inadaiwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Ole Lenga alikutana nao
> usiku na kuwataka wahakikishe wananchi hawatoi mabango, walifikisha kilio chao kwa waandishi wa habari.
>
> Wananchi hao walidai kuwa wamechoshwa na kunyanyaswa na mkuu wa wilaya hiyo
> hasa wanapofuatilia haki zao kwa madai kuwa hawatapata chochote na watatembea hadi soli za viatu ziishe kwa lengo la kupata haki zao.
>
> Wakati huo huo katika hali isiyo ya kawaida na ambayo imezua maswali mengi ni
> kitendo cha mkuu wa wilaya hiyo kuamuru mwandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo mkoani hapa, Augustine Mgendi kukamatwa kwa madai kuwa alikuwa akiwachochea wananchi waandike mabango kuhusu malalamiko yao.
>
> Kitendo hicho kinadaiwa kililenga kuwanyamazisha wananchi na waandishi
> wasiibue uozo huo ambao umeishagharimu serikali karibu Sh 2 bilioni kwa
> ajili ya fidia, fedha ambazo zinaishia mikononi mwa wajanja na kuwaacha
> walengwa.
>
> Hata hivyo, mwandishi huyo aliachiwa baada ya kuhojiwa
> kwa saa zaidi ya nne na Jeshi la polisi na ikiwa ni pamoja na juhudi za
> waandishi kufuatilia kwa karibu. Hata hivyo, hakufunguliwa jalada.
>
> Kwa zaidi ya mara mbili serikali imeishatoa fedha kwa ajili ya kulipa fidia
> wananchi hao, malipo ambayo yanadaiwa kutawaliwa na ufisadi kwa baadhi
> ya viongozi kujiingiza ndani na kuwalipa wasiokuwa na maeneo na ambao
> wengi ni wafanyabiashara.
>
> Kwa mara zote hizo mbili msimamizi mkuu wa malipo hayo ni mkuu wa wilaya
> hiyo na timu yake.
>
> Akizindua mradi huo uliogharimu zaidi ya Sh10 bilioni, Rais Kikwete alisema kuwa
> ametimiza ahadi yake aliyoitoa wakati anagombea urais 2005 ya kukamilisha bwawa hilo.
>
> Alisisitiza utunzaji wa bwawa hilo utasaidia uhai wake kuendelea kwa muda mrefu, kwa kuwa likitunzwa vema huenda likadumu kwa zaidi ya miaka 50.
>
> “Kuoga, kunywesha mifugo humo ni marufuku kwa kuwa maji hayo yanatumika kwa ajili ya kunywa na serikali kwa sasa ina mpango wa kuhakikisha inajenga mtambo wa kutibu na
> kusafisha maji,”alisema Rais Kikwete.
>
> Alisisitiza uundaji wa kamati za maji huku akisisitiza kuwa wanawake wawe wengi, kwa kuwa miradi iliyosimamiwa na wanaume matokeo yake yamekuwa si mazuri.
>
> Mapema Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya akitoa taarifa
> fupi ya mradi huo alisema, mradi huo umejengwa kwa fedha za serikali na umegharimu Sh10.2 bilioni na lina lita za ujazo milioni 14.2
>
> Hii si mara ya kwanza kudanganywa kwani rais ameshadanganywa zaidi ya mara kumi mojawapo ikiwa ni ile ya kudanganywa kwamba, Daraja la Mkenda lililopo Ruvuma ambalo ni njia muhimu kuelekea Msumbiji, lilikuwa limekamilika.
>
> Kutokana na hali hiyo, Rais alilazimika kukatisha safari yake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Monica Mbega, (wakati huo)ambaye alionekana pia kutofika katika daraja hilo kabla.
>
> Katika tukio jingine, Rais aliwahi kupewa taarifa zisizo sahihi kuhusu tuhuma za rushwa zilizokuwa zikimkababili Anatory Choya kisha akamteua kuwa Mkuu wa Wilaya, lakini siku siku chache baadaye akafunguliwa mashitaka na Takukuru.
>
> Mwaka jana, akiwa ziarani Mbeya Rais msafara wake ulishambuliwa kwa mawe na watu, lakini wasaidizi wake wakaja kutoa taarifa kwamba watu hao walikuwa ni wahuni na walikuwa walimsubiri Rais kwa muda mrefu bila mafinikio.
>
> Hata hivyo, baadaye uchunguzi huru ulibainisha kwamba tukio hilo lilikuwa na mafungamano ya kisiasa na makovu ya mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM kwa mwaka 2005.
>
> Mlolongo huo mrefu wa upotoshaji taarifa kwa Rais uliibuka tena katika utoaji wa magari ya misaada, ambako badala ya kupewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido alipewa wa Ngorongoro.
>
> Tukio hilo lilimfanya mkuu huyo wa nchi kufura na kumzodoa mkurugenzi huyo, lakini baadaye ikabainika mkurugenzi huyo alikwenda kutokana na makosa ya maafisa wa Ikulu.
>
> Katika mlolongo huo, tukio kubwa kabisa ni Rais kutia saini kwa mbwembwe Sheria ya Gharama za Fedha za Uchaguzi ambayo ilichomekwa vipengele nje ya Bunge kitu ambacho ni kinyume cha sheria.
>
> Tukio hilo ambalo ni la uvunjifu wa katiba, liliibuliwa na Katibu Mkuu waChadema, Dk Willibrod Slaa ambaye awali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fedrerick Werema, alikanusha.
>
> Hata hivyo, baadaye sheria hiyo ilirudishwa bungeni na kukarabatiwa kwa mgongo wa mabadiliko ya sheria mbalimbali.
>
> Mei mwaka huu, Rais alipewa taarifa za upotoshaji kuhusu mazungumzo ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) na serikali, kwa kuelezwa shirikisho hilo halikuhudhuria mkutano wa saa 4:00 asubuhi kama ilivyopangwa.
>
> Hata hivyo, Tucta wakatoa ushahidi wa barua za mwaliko wa mkutano huo wa Aprili 22, ambazo zilikuwa mbili moja ikionyesha walitakiwa kufika katika mazungumzo
> Hazina saa 4:00 asubuhi na nyingine saa 8:00 mchana.
>
> Katika kuonyesha upotoshaji kwa Rais, wasaidizi hao walimpa barua iliyokuwa
> ikionyesha walipaswa kukutana saa 4:00 asubuhi huku ile ya saa 8:00 wakawa wameificha.
>
> Rais akizungumza na wazee wa mkoa wa Dares Salaam aliwashambulia viongozi wa Tucta hasa Naibu Katibu Mkuu Nicolas Mgaya, akimwita mnafiki, mzandiki, mchochezi na hiana.
>
> Wakati huo huo ahadi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa aliyowahi kuitoa Rais
> Kikwete kuwa utajengwa Serengeti ameshindwa kusema utaanza lini.
>
> Rais Kikwete akiwa ziarani wilayani humo aliwahi kusema kuwa Serikali
> itajenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wilayani hapo kwa ajili ya
> kurahisisha usafiri kwa watalii na kukuza uchumi wa wilaya na taifa.
>
> Akihutubia wakazi wa mji wa Mugumu na viunga vyake wakati wa uzinduzi wa
> mradi wa bwawa la Manchira, Rais Kikwete alisema kuwa ahadi yake iko pale pale kuwa utajengwa.
>
> Alisema kuwa uwanja huo licha ya kukabiliwa na vikwazo vingi ikiwemo taarifa kutoka kwa nchi jirani kuwa kujengwa kwa uwanja huo kutasababisha nyumbu kutoa mimba kwa wingi.
> “Maneno ni mengi kuhusu uwanja huo, lakini nasema ahadi iko pale pale, tutajenga na
> huenda nyumbu wakaongezeka maana hayo si maneno ya kitaalam, maana wageni wanapata shida sana hapa, wanateremkia Kilimanjaro, wanakuja kwa magari, lazima tujenge,” alisema bila kufafanua ni lini.
>
> Kuhusu barabara ya lami kutoka Makutano hadi Tabora kupitia Hifadhi ya
> Serengeti alisema itajengwa kwa baadhi ya maeneo ambapo kilometa 50 ndani ya hifadhi hazitajengwa ili kuhifadhi mazingira.

No comments:

Post a Comment