Sunday, July 4, 2010

KWAHERI UKOLONI, KWAHERI UHURU (SHAIRI)

Sehemu ya Tatu SOMA KUANZIA CHINI SEHEMU YA KWANZA HADI HAPA. IMECHANGIWA NA BWNATOSHA WA UFARANSA. Salim H. Bwanatosha
Paris, France
(L/Line:+331-74301059;Mbl:+336-27146412)


21.
Kwa yote yanayosemwa
Kitabuni kutetema
Tarehe haijatemwa
Harithi anabaini!
22.
Harithi anabaini
Kutwambia kwa yakini
Ya mazito na laini
Ushirazi na Mwambao!
23.
Ushirazi na Mwambao
Bara Hindi na Hiyao
Mrima kwetu kwao
Barawa hata Nosy Be!
24.
Barawa hata Nosy Be
Bukini na Darugubey
Wadebuli na Wa-Pate
Uswahili ndo mkate!
25.
Uswahili ndo mkate
Zinjibari tupakate
Temedeni tuzipate
Sote ni waja wa M'Ngu!
26.
Sote ni waja M'Ngu
Kuvamiwa na Mzungu
Tufinyange zetu nyungu
Unguja na yetu Pemba!
27.
Unguja na yetu Pemba
Taifa-Dola kubeba
Kwa vikoi na vilemba
Watwani usende tete!
28.
Watwani usende tete
Makunduchi hata Wete
Ni kama Chanda na Pete
Chuki nyingi ni za nini?
29.
Chuku nyingi ni za nini?
Shetani kutuzaini
Ungwanetu kuukhini
Zinjibari kwenda pogo!
30.
Zinjibari kwenda pogo
Si wa chai si muhogo
Badili pua na chogo
Tu'auni Bwana M'Ngu!
----------
"Aliyesifu ugari, huyo ni mpuuzi
Bila ya mchuzi, huuli mtupu ugari!"

Afrabia ndio yetu
Swahilini ndiko kwetu
Tusitupe kilo chetu
Kwa watu waso wenzetu!

Sefu na wetu Amani
Wamesokota kamani
Saa yetu ikhiwani
Itawadi kwetu Pwani!

Tushangirie ukweli
Uchaguzi kuwa meli
Ya kabwela na kubeli
Kwa Karume na Mugheiry!
------------
Wama 'ala Rasul Ila-l-Balaghu-l-Mubiin!

Salim H. Bwanatosha
Paris, France
(L/Line:+331-74301059;Mbl:+336-27146412)


From: bwanatosha@hotmail.com
To: afrabia@gmail.com

Sehemu Ya Pili

11.
Maudhu'i si kidogo
Chimbuko umbua pogo
Harith ni Mwana Jogoo!
12.
Atwambia za Mzungu
Kufita yetu matungu
Ngezi, Nungwi, Takaungu!
13.
Tuchimbue historia
Nyongo na mbovu fagia
Wana tupate wambia!
14.
Tuweze sogea mbele
Ponyesha zetu ndwele
Mashina hata vilele!
15.
Simisha yetu IMANI
Sefu na khasa Amani
Kuwashinda maruhani!
16.
Hawa ni kweli vigogo
Wapambe sura na chogo
Kufinyaza vyombo dongo!
17.
Tataga uzi wa M'Ngu
Hizbu na Afro mbumbumbu
Umma na Nduwaro maumbu!
18.
Na zetu kweli tabia
Sote tuweze sikia
Zahitaji manabia!
19.
Tuwache hizi kelele
Tupate pika mchele
Taifa lisonge MBELE!
20.
Sote tuwe IKHIWANI
Wana sote wa Watwani
Tula'ani SHAITWANI!
----------
Salim H. Bwanatosha
Paris, 23/06/10

--------------------------------------------------------------------------------
Sehemu Ya Kwanza

01.
Hakika, lelo, ndo naanza
Mapesi kusoma na kuwaza
Ha kukanguwa nto mapanza
Kwa elimu inu ya kwanza!
02.
Kwa elimu inu ya kwanza
Zenjibari ilipoanza
Maji mema ya kutawaza
Kuwa na Taifa letu sote!
03.
Kuwa na Taifa letu sote
La michango kutoka kote
Tusiwe na khofu yoyote
Marithi ni ya wana wote!
04.
Marithi ni ya wana wote
Tindo, haiba, kote kote
Na kujifahari kwa yote
Hayo tuyajue yakini!
05.
Hayo tuyajue yakini
Ghassany weledi makini
Atupa tarehe 'aini
Ya kujenga matumaini!
06.
Ya kujenga matumaini
Tusije katika maini
Taifa-Dola kulikhini
Poteza muruwa na CHEO!
07.
Poteza muruwa na cheo
Mwinyi, Sultani, mambo leo
Walaji wingi vitoweo
Kwa ukali na makemeo!
08.
Kwa ukali na makemeo
Unguja hata Kiwa Ndeo
Watubane kwa makoleo
Kukana uweza wa M'Ngu!
09.
Kukana uweza wa M'Ngu
Kwa kupika yao majungu
Watapa tapa na mikungu
Na kuenda mbio za nyumbu!
10.
Na kuenda mbio za nyumbu
Kwa kukimbia kumbu kumbu
Vichwa mchangani kuumbu
Zanzibar si sawa na MBU!

No comments:

Post a Comment