> URAIA WA NCHI MBILI WAKUBALIWA KITAIFA
Jul 5, 2010
>
> Serikali imekubali kuwepo kwa uraia wa nchi mbili kwa Wabongo walioko nje ya
> nchi na kwamba wasichukuliwe kama wasaliti.
>
> Kutokana na hatua hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
> iko kwenye mchakato wa kuwasilisha muswada kuhusu uraia wa nchi mbili kwenye
> kikao cha Baraza la Mawaziri.
>
> Hayo yalisemwa juzi mjengoni 'Bungeni' na Waziri wa Mambo ya Nje na
> Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe.
>
> Waziri Membe alisema siyo dhambi, Watanzania kutafuta riziki nje ya nchi na
> ni haki yao kubaki na uraia wa Tanzania.
>
> Alisema wakati umefika kwa Watanzania, kupatiwa haki yao ya msingi kwani
> licha ya kuwa ni manufaa kwao pia ni manufaa kwa nchi kutokana na fursa ya
> kuongeza pato la taifa.
>
> "Tusiwaangalie Watanzania walioko nje ya nchi kama wasaliti, watu hawa ni
> raia wema lakini walikwenda kutafuta riziki tu ili wachumie juani na kulia
> kivulini, hivyo tunapowafutia uraia wa ndani hatuwatendei haki,".
>
> Alisema kama Tanzania imeweza kutoa uraia kwa wakimbizi 169,000 kutoka
> Rwanda na Burundi, haiwezi kushindwa kuwabakishia uraia wao wananchi wake
> wanaokwenda kutafuta nje ya nchi.
>
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDelete