Saturday, January 17, 2009

TUMBAKU ILIYOIBWA MOROGORO YAKAMATWA SALALAH, OMAN

Jamani, Polisi wa Tanzania wangekuwa makini ndani ya nchi yetu kiasi hiki, bila shaka uhalifu ungepungua sana na watu kupata haki/mali zao zilizoibiwa.

John Nditi, Morogoro
Daily News; Wednesday,January 14, 2009 @20:00
Polisi nchini kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa, ‘Inter Pol’ wamefanikiwa kukamata marobota 990 ya tumbaku yenye thamani ya Sh bilioni 1.2. Marobota hayo ambayo yanadaiwa kuibwa kutoka kiwanda cha tumbaku cha TTPL yalikamatwa katika bandari ya Salalah, Oman.

Wizi wa marobota hayo ulifanyika Oktoba 25, 2008 na kuripotiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Morogoro, Novemba 18, 2008. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye, alisema juzi mjini hapa kuwa kwa kushirikiana na wenzao wa walifuatilia nyendo za wizi huo katika bandari mbalimbali na hatimaye kuweza kuyakamata marobota hayo katika Bandari hiyo ya Salalah iliyopo nchini Oman.

Alisema marobota hayo 990 yalikamatwa Desemba 17, mwaka jana na kurudishwa nchini Januari 9, mwaka huu ambapo shughuli za upakuaji zilianza Januari 11, mwaka huu kurudishwa mkoani hapa. Kamanda huyo alisema malori makubwa 10 yalitumika kwa ajili ya kubeba makontena yaliyosheneni marobota hayo yaliyokamatwa na Polisi wa kimataifa.

Hata hivyo, alisema bado uchunguzi wa kina juu ya wizi huo unaendelea kufanyika ili kuweza kubaini mazingira ya wizi huo ambao awali uliripotiwa katika kituo hicho cha Polisi. Kamanda Andengenye amesema kwamba Polisi kwa sasa wanaomba kibali cha mahakama ili kuangalia kama tumbaku hiyo bado inafaa kwa matumizi ya kawaida.

No comments:

Post a Comment