From Zimbawe dated 14/9/2012
Harusi ya Tsvangirai yasitishwa:
- So he is being accused of an inchoate crime of bigamy?? Or what?
Tsvangirai na mpenzi wake
Mahakama
 nchini Zimbabwe imesitisha harusi ya Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan 
Tsvangirai iliyotarajiwa kufanyika hapo kesho kama ilivyokuwa imepangwa.
Mahakama imesema kuwa Tsvangirai tayari ana mke.
Mapema
 wiki hii mahakama kuu nchini humo ilitupilia mbali madai ya Locadia 
Tembo aliyesema kuwa yeye ni mke wa kitamaduni wa Bwana Tsvangirai na 
kusema kuwa ndoa za kitamaduni hazitambuliki kisheria.
Lakini sasa
 Hakimu amekubaliana na Locadia na kuamuru harusi iliyopangwa kufanyika siku ya Jumamosi haitafanyika tena.
Hii ni licha ya baadhi ya viongozi wa nchi mbali mbali walioalikwa kwa harusi kuwasili nchini humo.
Mawakili wa Tsvangirai wanataka mahakama kutoa amri ya dharura na kuruhusu harusi hiyo kuendelea kama ilivyopangwa.
Kesi
 nyingine ambayo mahakama ilisikiza leo dhidi ya Tsvangirai ni ya 
mwanamke mmoja kwa jina Nozipho Shilubane aliyesema kuwa Waziri Mkuu 
huyo aliahidi kumuoa.
Baadhi ya wadadisi 
wanasema kuwa kesi hiyo ni dalili ya njama za kisiasa kumpaka tope 
waziri mkuu kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka ujao. Tsvangirai 
atatoana jasho na rais Robert Mugabe katika uchaguzi huo.
Lakini
 wengine wanasema kuwa Tsvangirai hana wa kulaumu ila yeye mwenyewe 
kwani amejihusisha na wanawake wengi baada ya mke wake kufariki katika 
ajali ya barabarani mwaka 2009 baada ya waziri mkuu kuchukua wadhifa 
wake.
Mwandishi wa BBC Brian 
Hungwe mjini, Harare, anasema kuwa harusi hiyo ilipangwa kufanyika 
katika mtaa mmoja wa kifahari mjini Harare.
Rais Mugabe anatarajiwa kuandaa dhifa maalum kwa viongozi wa nchi za kiafrika walioalikwa kuhudhuria.
 
 
No comments:
Post a Comment