Imeingizwa hapa tarehe 13/9/2012.
Imesomwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, FREEMAN MBOWE, Tarehe 10 Septemba, 2012.
1. Uwajibikaji wa kisiasa wa viongozi wa serikali na idara zake.,Waziri
Emmanuel Nchimbi, IGP Saidi Mwema, Paul Chagonja, RPC Morogoro, Kamanda wa FFU,
RPC IRINGA na Kamanda wa FFU wajiuzulu na/au wafukuzwe kazi.
2.RPC Morogoro na Iringa, makamanda wa FFU Morogoro na Iringa, Askari waliouwa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka.
3.Rais aunde tume huru ya uchunguzi wa vifo tata katika matukio yA kisiasa.
1. ARUSHA vifo 3.
2. IGUNGA,vifo vingi havijulikani bado,
3. ARUMERU MASHARIKI, vifo 5,
4. SINGIDA kifo 1,
5. MOROGORO kifo 1, 18 Agosti, 2012.
IRINGA kifo cha Daudi Mwangosi, Mwandishi wa Habari wa Channel Ten, 2 Septemba, 2012.
CHADEMA haitatambua wala kushirikiana na kamati batili ya NCHIMBI.
4.Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa ni mtu hatari kwa taifa kwa kauli
tata anazozitoa.anashirikiana na au anajipendekeza kwa CCM na Serikali
yake.CHADEMA tangu sasa haitafanya kazi na Tendwa wala kufanya mawasiliano
naye ya kiofisi.Labda kama atagundua makosa yake na kuomba msamaha,
CHADEMA itatafakari namna ya kufanya naye kazi tena.
5.TBC TAIFA Television na Redio ni hatari kwa taifa,kwa kubobea kupotosha
umma juu ya matukio mengi.Hivyo CHADEMA Inatangaza mgogoro na TBC na
inaelekeza na kuomba wanachama ,wapenzi,na wananchi wote wapendao ukweli na
haki,kuisusia TBC
6.Jeshi la Polisi lijue kuwa Maandamano ndiyo siasa yenyewe na mikutano ya hadhara ni lazima kwa
mawasiliano ya umma na siasa.kuzuia vitu hivyo ni
kunyima wananchi haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kukusanyika na kutoa
maoni,pia kupata habari na taarifa
7.Operesheni MOVEMENT FOR CHANGE M4C,Inaendelea kadiri ya ratiba
ilivyopangwa katika utaratibu uleule uliokuwepo awali.Inarejea Iringa Siku si nyingi.
Na kamati kuu Imetoa msisitizo MAALUM kwa jimbo mojawapo
singida,ambapo wamesema watatumia helcopita,magari,pikipiki na baiskeli na
miguu,na badala ya kupita vijijini kama majimbo mengine,Chadema wanasema kwa
sababu maalum katika jimbo hilo watapita kitongojikwa kitongoji,ili kufunza
adabu baadhi ya viongozi (msisitizo ni wa msoma MAAZIMIO.jimbo hili laweza
kuwa la Mwigullu Mchemba,kadiri ya wanahabari waliokuwepo)
8.Kutokana na mgogoro wa muda mrefu mkoani mwanza uliosababisha meye wa
chadema kuvuliwa umeya kinyume na utaratibu na kwa njama za CCM na
Serikali,na bahati mbaya sana kwa kushirikisha madiwani wa CHADEMA,KAMATI
KUU imewavua UANACHAMA madiwani wake wawili 1 ADAMU CHAGULANI wa kata ya
IGOMA na HENRY MATATA wa KITANGIRI, PIA uongozi wote wa CHADEMA mkoa wa
Mwanza Umevunjwa.
No comments:
Post a Comment