Thursday, September 6, 2012

JAJI MKUU WA TANZANIA AUGUSTINO RAMADHANI

Tofauti ya Majaji wa Tanzania na Marekani ni kwamba, Majaji wa Tanzania wana umri wa Kustaafu kikatiba (miaka 60); kufuatana na Ibara ya 110(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; wakati Majaji wenzao wa Marekani, hawastaafu hadi washindwe wenyewe, ama kwa uzee au kwa udhaifu wa ugonjwa.

Friday, July 20, 2007


Jaji Mkuu Mpya wa Tanzania, Brigedia Jenerali Augustino Ramadhani

Rais Jakaya Kikwete Julai, 19 2007 amemwapisha Jaji Augustino Ramadhani kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, baada ya Jaji Mkuu Barnabas Samatta kustaafu rasmi. Jaji Ramadhani amewahi kuwa Jai katika mahakama ya Afrika Mashariki ambako alikuwa yeye na Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba. Sambamba na kuwa mwanasheria na mwanajeshi, Jaji Ramadhani pia ni mpiga kinanda maarufu katika kwaya ya Kanisa la Anglikana jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu Augustino Ramadhani amerithi kiti alichokalia kabla yake Jaji Barnabas Samatta, Jaji Francis Nyalali, hawa wote ni Wazalendo wa Tanzania. Kabla yao, kulikuwa na Jaji Goerges, alikuwa mgeni.

No comments:

Post a Comment