Date: Thursday, May 14, 2009, 3:44 PM
TEMBO, NYUMBU WA KENYA WAHARIBU MAZAO KILIMANJARO |
Written by Rehema Matowo | |
MKUU wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Anarose Nyamubi ameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuwaondoa wanyama wakali kutoka nchini Kenya waliovamia makazi ya watu katika Wilaya hiyo na kusababisha wakazi wa maeneo hayo, kuogopa kutoka nje kwa kuhofia kujeruhiwa na tembo na nyumbu. Nyamubi aliyasema hayo, katika kikao cha 18 cha ushauri cha Mkoa kilichofanyika juzi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na kufafanua kuwa kundi la Nyumbu, tembo na swala kutoka katika msitu wa hifadhi wa Amboseli nchini Kenya wamevamia katika Wilaya hiyo na kuharibu mazao ya chakula. UNAONA BASI, HATA WANYAMA WA KENYA WANATAKA KUHAMIA TANZANIA! Jitukali. |
No comments:
Post a Comment