Tuesday, May 12, 2009

ASKARI WA MAR kwamba askari Mpiganaji huko Camp Liberty, kambi ya jeshi la nchi ya Marekani iliyopo EKANI IRAQ WAPULULANA

Niliwahi kusema humu katika makala za nyuma kwamba kauli ya mama mmoja wa kule Gettysburg, Pennsylvania, Bi Amy V. Linenberger aliyoniambia tarehe 18 Aprili, 2009; kwamba hakuna mshindi katika vita, haikuwa kauli ya kebehi. Ilikuwa kauli ya kweli na ni kweli tupu.



Haya yanathibitishwa na habari ya leo hii katika gazeti la "USA TODAY" Jumanne, Mei 12, 2009 iliyotokea karibu na Uwanja wa Ndege wa Baghdad, nchini Iraq, askari wa Marekani kawafyatulia risasi na kuwauwa wenzie watano kwa mpigo. Jeshi la nchi hiyo halikutoa jina la Mpiganaji huyo aliyepulula wenzie wala majina ya Wanajeshi wa Marekani watano waliouwawa na mwenzao. Serikali ya nchi ya Marekani sasa hivi inatafakari hatima ya askari wapatwao na Masononeko, Misongo ya Moyo (Post traumatic stress disorder- PTSD) na Majakamoyo kwamba wanafikia hali ya kupululana namna hii; pamoja na kupatiwa matibabu na wataalam wa matatizo hayo ya akili.



Habari hii imetoa takwimu za matukio kama haya ya kuuwana wenyewe kwa wenyewe wakiwa vitani huko Iraq kwenye vita ambayo Wamarekani wameipachika jina la "Operation Iraqi Freedom", iliyoanza Machi 20, 2003 chini ya utawala wa Rais George Walker Bush, kama ifuatavyo:



1. Machi, 2003, Askari Makamanda wawili wameuwawa, na wapiganaji 14 walijeruhiwa huko nchini Kuwait, nchi inayopakana na Iraq.



2. Juni, 2005, Sajenti mmoja alipigwa risasi na kufa mjini Baghdad.



3. Novemba, 2005, askari aliuwawa mjini Baqouba, Iraq na Mhudumu wa afya Jeshini.



4. Sepemba, 2007, Askari mmoja aliuwawa kwa risasi mjini Baghdad, na mwenzie amekiri kuuwa (voluntary manslaughter).



5. Oktoba, 2007, Askari wawili wanamaji wameuwawa mjini Bahrain. Askari mwingine mwanamaji aliyeshukiwa kuhusika na tukio hilo alijitungua mwenye kwa risasi akaumia.



6. Septemba, 2008, Askari wawili waliuwawa mjini Tunnis, Iraq, mmojawao katika Platuni akashitakiwa kwa uhalifu huo.



7. Jumatatu, Mei 9, 2009 ndio hii habari kubwa ya askari kuuwa wenzie watano hapo Baghdad.



Hadi kufikia hiyo Jumatatu, askari 4,276 wapiganaji, na wafanyakazi wa wizara ya ulinzi 11 wametambuliwa rasmi kuwa wameuawa katika vita vya Iraq; 3,440 kutokana na adui, na 847 kutokana na matukio yasiyohusiana na mapambano.



Habari hiyo imesema askari wa mwisho kutambuliwa kufa katika orodha hiyo ni Sajenti Randy S. Agno (29) aliyekuwa Ijumaa, Mei 8, 2009 katika hospitali ya Jeshi ya Walter Reed iliyopo Washington DC. Marehemu huyu alifia vidonda alivyopata Aprili 27, 2009 alivyovipata katika tukio lisilohusiana na vita huko "Forward Operating Base Olsen mjini Samarra, Iraq. Kijana huyu mdogo alikuwa anatokea jimboni Hawaii na alikuwa katika kikosi cha Askari wa Miguu (Infantry) Divisheni ya 25.

Hivi niandikavyo, haijulikani lini wala wapi vita hii itamalizika. Hivyo ni wazi kuwa tutarajie ongezeko la idadi ya Majeruhi na Wafu katika vita hii kwa pande zote mbili. Kwa upande wa Iraqi, waliouwawa hadi sasa wameshavuka mamilioni, hawa ni raia pamoja na Wanajeshi. JE, TUNA SABABU YOYOTE YA KUSHUKU ZAIDI KWAMBA HAKUNA MSHINDI VITANI?

No comments:

Post a Comment