Saturday, May 2, 2009

MBWA KUENDELEA KUWA " PET" KAMA "MTOTO"

Mambo haya yanatokana na wenzetu kuwafanya mbwa kama watoto wao majumbani. Maendeleo yamewafanya wenzetu wathamini wanyama zaidi ya kuthamini binadamu wenzao. Mimi haya siyaiti maendeleo asilani, huku ni kukosa utu kabisa. Kama alivyofanya mama mmoja huku Marekani kwa kumsakizia mbwa wake wawili jirani yake eti tu kwa sababu walikosana mwaka jana 2008. Mbwa wale walimushambulia jirani yake wakati yeye akishuhudia hadi jirani yake akafariki palepale. Naona aliwapongeza mbwa wake na kujipongeza mwenyewe. Mahakama nchini humu ilimhukumu mama huyu miaka 16 jela kwa kosa hili.

Bora huyu wa habari hii aliyeamuru mbwa wake waliogeuka NUNDA kuuwawa, ameonyesha kwamba mtu ni bora kuliko mnyama.

Man dies following attack by dogs

A man who was savaged by two Alsatian dogs has died, police said. Skip related content

Related photos / videos

A man has died after an attack by two alsatian dogs, police have confirmed.

The man, 21, was bitten by the dogs when he tried to separate them during a fight at his home in Reads Avenue, Blackpool, at about 8pm on Friday.

Lancashire Police said he was bitten and then fell and hit his head, which they suspect caused his death.

He lived at the property with the dogs' owner.

Inspector Simon Atkinson of Lancashire Police said: "Both turned and made a sustained attack on him, making puncture marks on his upper body.

"The owner of the dogs intervened and the dogs were dragged away."

Mr Atkinson said police believed the man may then have fallen over several times and banged his head.

He said he collapsed and died shortly afterwards, despite the intervention of paramedics.

The cause of death has not been established and a post-mortem will be carried out.

The two dogs have been destroyed at the direction of their owner.

1 comment:

  1. Nimetumia miaka mingi kutafakari tofauti za tamaduni zetu waAfrika kulinganisha na utamaduni wa waMarekani. Mwanzoni, nilikuwa nawaona waMarekani kama watu wa kushangaza tu. Niliona hawana heshima, hawana utu, na kadhalika.

    Lakini kadiri miaka ilivyokuwa inapita, nilianza kutambua kuwa nilichokuwa nafanya ni kutumia vigezo vya utamaduni wetu waAfrika. Pole pole nikaanza kutambua kuwa kwa mtindo huo, Mmarekani naye anaweza kutuangalia sisi kwa kutumia vigezo vya utamaduni wake, akatuona hatuna heshima, hatuna utu, na kadhalika.

    Na ukweli ni kuwa waMarekani wanapotuona tunavyowapiga mbwa, kwa mfano, anasikitika, na kutuona hatuna utu. Lakini kwetu sisi, mbwa hata hatumlishi vizuri, bali tunamwacha ahangaike mwenyewe maporini au kwenye majalala. Wamarekani hawafanyi hivyo, na wanaweza kutuona sisi katili.

    Jukumu linalotukabili katika dunia ya leo ni kujitahidi kuzifahamu tamaduni mbali mbali na misingi yake, na wao watufahamu, na labda tutafikia maelewano kwamba tamaduni zote zina misingi yake na mantiki yake. Nimeandika kitabu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, ambamo nimeelezea mengi ya aina hiyo.

    ReplyDelete