Tuesday, May 5, 2009

MAITI AGUNDULIWA BAADA YA MIEZI 18

Death That Nobody Noticed: Haya ndio maisha ya wenzetu wa nchi ya Marekani. Marehemu bibi huyu hakuwa akiishi porini. Ni mjini, lakini hakuna aliyefahamu kwamba keshafariki hadi hiyo miezi 18 kupita, yaani zaidi ya mwaka mmoja na nusu. Ni wazi kwamba hali ya hewa ya nyumba yake iliruhusu kuhifadhi kwa maiti yake muda wote huo vinginevyo wangekuta mifupa mitupu. Habari hii haikueleza endapo maiti iligunduliwa vipi, lakini majirani zake wanashangaa kwamba walikuwa wanaishi na mfu jirani yao kwa muda wote huo.

Haya andio maisha ya huku. Kwamba jirani yako hana habari na wewe na wewe huna habari na jirani yako zaidi ya kusema tu "hi" mkutanapo barabarani. Hata majina huku majirani hawajuani hata ukiishi na jirani kwa miaka dahali. Yaani maendeleo yamewafanya wenzetu wawe WAPWEKEPWEKE kiasi hiki. Hakutokea hata jirani wa kumuuliza jambo tu ile ya kusalimia marehemu huyu vinginevyo maiti yake ingegunduliwa mapema zaidi ya miezi 18.

Kauli ya huyu jirani kwamba angemjulia hali jirani yake kama angejua kwamba hakuna anayefanya hivyo ni kustarehesha baraza tu. Kwa sababu kumjulia hali mtu/jirani sio lazima ujue kwamba hakuna anayemjulia ndio wewe ufanye hivyo. Ujirani hautakiwi kuwa wa kuvizia nani kampa jambo ili mimi nisimpe. Ni wajibu wa majirani kujua hali za majirani zao lakini sio Marekani.
Hivyo ndugu zangu Waafrika, tafadhali fikirieni mara mbili mnapoamua kuzamia au kupata sababu halali za kuishi katika nchi kama hii, kwa sababu utamaduni wao ni kinyume na ule tuliouzoea wa kila jirani kumjulia hali jirani yake na hivyo kujua kinachoendelea mtaani au kijijini.

DEATH THAT NOBODY NOTICED!

Mary Sue Merchant, 74, died of natural causes in her Orangeburg, South Carolina home 18 months before her body was found in March, 2009. Her electricity was cut off, and her property had even been sold at auction after taxes went unpaid. "It just blows my mind," a neighbor told a local paper, saying she would have checked in on her had she known nobody else was.

No comments:

Post a Comment