Thursday, October 11, 2012

MAONI YA KATIBA MPYA TOKA KWA IDRISA FAIDA, TANZANIA

Yameingizwa humu leo hii 11/10/2012.

MAONI YA KATIBA MPYA


1. Wananchi waliopo kwenye maeneo yenye rasilimali za taifa wanufaike moja kwa moja kwanza kutokana na rasilimali hizo.

2. Kutokana na ufisadi, mmomonyoko wa maadili, kukithiri kwa rushwa, ngono, utapeli na mengine mengi yanayotokana kutokuwa na hofu ya Mungu katiba iruhusu mfumo wa elimu wa kidini ili kujenga maadili ya viongozi wa baadae wenye hofu ya kudhulumu wengine.

3. Nafasi za ziongozi katika sekta za kiserikali , katiba mpya itamke wazi kuwa kuwe na uwakilishi wenye uwiano sawa kwa dini zote, (wakristo, waislam)

4. Katiba mpya isiruhusu mkataba wowote kati ya mtu mmoja na nchi/ jamii moja na nchi au mtu mmoja na mwingine kwa niaba ya kuwakilisha watanzania wote badala yake mikataba yote ipitie bungeni au chombo maalum cha kupitisha mikataba kabla ya kusainiwa kwake (chini ya wanasheria).

5. Katiba mpya iruhusu jamii ya kitanzania kujiunga na mashirika ya ndani naya nje kwa maslahi ya jamii husika na kwa watanzania wengine kwa ujumla.

6. Kutokana na mwiingiliano na mkanganyiko wa kuutendaji kati ya serikali ya jumuhuri ya muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, katiba ijayo iruhusu uundwaji wa serikali tatu

 (i) serikali ya Tanganyika,
(ii) serikaili ya mapinduzi Zanzibar na
(iii)SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

7. Katiba itamke rasmi kuwa ngazi za urais katika Selikali ya Muungano wa Tanzania ni wa kupokezana kwa uadilifu. Mfano Rais akitoka bara makamu wa rais atoke Zanzibar, kipindi kijacho rais ni Zanzaibar na makamu atakuwa wa kutoka  Tanzania Bara.

8. Katiba iwatambue wanandoa (mke na mume) wenye jinsia tofauti pekee.

9. Katiba mpya iruhusu na kusimamia watanzania kuhukumiana kimila, kijamii au kidini iwapo jambo wanalohukumiana halina ufafanuzi wa kina au kukosa wataalam wa undani katika mahakama za kiserikali, hivyo basi mahakimu wa mahakama hizo watumike katika kutatua masuala hayo.

10. Katiba isiruhusu mkataba wowote wenye mrengwe wa kubaguzi katika kuwaga watanzania kimikoa, kikabila wala kidini kwa kuupendelea jamii moja, dini moja au mkoa mmoja kinyume na mingine.

11. Iwapo kutauwa na mkataba wowote wenye misingi ya kibaguzi wa kiamajimbo,jamii na kidini katiba itamke wazi kuvunjwa kwa mikataba hiyo.

12. Katiba mpya iruhusu mgombea binafi katika nafasi mbalimbali isipokuwa ngazi ya urais pekee.

13. Katiba mpya iruhusu uundwaji wa mahakama kuu ya katiba ili kusimamia utekelezaji wa sheria za nchi.

14. Kutokana na Tanzania kuwa ni mwanachana wa umoja wa mataifa aliyesaini kuunga mkono haki za binadamu, sheria zote zenye kupingana na haki za binadamu zisiwekwe kwenye sheria mpya.

15. Mwenye kuthibitika kuuwa kwa maksudi sheria ya kifo iwe ni halali kwake. ( Sheria ya kifo itekelezwe ili kupunguza watu kuuana bila sababu ya msingi)



TANBIHI (ZINDUKA) Ndugu toa nakala kadri uwezavyo ili siku ya kuchangia kila mtu asome kutoka kwenye nakala yake asitokee mwananchi kudai yeye hana hoja ya kuchangia, maoni yetu baadhi ni haya.

No comments:

Post a Comment