Thursday, October 11, 2012

AFANYIA MTIHANI WODINI, MOROGORO, TANZANIA

Date: Wednesday, 10 October, 2012, 19:58

MWANAFUNZI  AFANYIA MTIHANI HOSPITALINI


Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Alfa Morogoro, Jesca Kiliani (17) akifanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne akiwa wadi namba 7B katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro jana 9/10/2012, baada ya kulazwa kufuatia kufanyiwa operesheni ya uvimbe ambapo hivi sasa anaendelea na matibabu hospitalini hapo.

[Shule hii ya Alfa ndio shule pekee Manispaa ya Morogoro inayotoa elimu ya Sekondari kwa watu wa rika lolote lile.   Mtu yeyote aliyeikosa elimu hii wakati wake anaweza kujiunga na shule hii ya sekondari na kuendelea na masomo ili mradi tu anamudu kulipia ada yake ambayo ni nafuu sana kwa sababu hugawiwa kadri mlipaji anavyoweza kumudu kuilipia. 

Shule hii ipo katika eneo la Mjimwema, Kata ya Nanenane, Manispaa ya Morogoro.]

Habari kamili: http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/26505-afanya-mtihani-kidato-cha-nne-wodini

No comments:

Post a Comment