Wednesday, October 13, 2010

UCHAGUZI TANZANIA 2010 MAMBO!

PIMAJOTO INAZIDI KUPANDA KWA KUSINGIZIWA WAPINZANI ETI WATAMWAGA DAMU? KWA KUTUMIA NINI?
WAMWAGAJI DAMU NI CCM TOKA KILOMBERO, MWEMBECHAI, PEMBA, etc.

Kwa nini wanatisha wananchi na wakati vyombo vyote vya mitulinga viko mikononi mwao? Someone is afraid - really afraid!!

By the way, ni utawala gani wanaofanya ambao Watanzania wengine hawawezi?
Kugawiana nyumba za serikali?
Kuiba fedha zetu BOT?
Kugawa mashirika yetu kwa wageni?
Kutumia bilioni 150 kwa mwaka kwenye usafiri wa Presidency?
Kujipangia mishahara ya milioni 10 kwa viongozi?
Kupeana sitting allowance za board meetings za 1 million per day?
Kuachia boda boda na mabasi kufanya barabara zetu ni machinjoni?
Kusinzia bungeni na kupiga piga makofi kwenye kila kikao?
Kuruhusu magogo na pembe za ndovu kupitishwa barabara zetu na kupakiwa melini na kupelekwa nje mchana mchana?
Kuhakikisha Tanzania na haswa Zanzibar imekuwa key transhipment ya drugs from the middle and far east to South Africa, Europe and US? Kuuziwa radar ya million 28 kwa 40?
Kushindwa kumaliza kesi yoyote ya EPA ambao ushahidi uko wazi tangu 2006?
Kuwaachia wageni kuendeleza kila sekta ya uchumi na kujisifu ndio maendeleo?
Kuwagawia watoto wa mfalme wa Saudia ekari mamilioni ya ardhi yetu kulima?
Kudumisha mgawo wa umeme tangu wakati wa Mkapa hadi leo?
Kuagiza kampuni feki (Richmond) ya kuuza vitabu kutununulia injini la ndege bovu feki eti kufua umeme?
Kwenda kununua mvua Thailand?
Rais kujiuzia mgodi wa mkaa wa mawe na mtambo wa kufua umeme Kiwira?
Kusimamia uchumi bei ya mchele toka 600 hadi 1500 in 4 years
Sukari toka 800 hadi 1600 (3000 Mbambabay) in 4 years?
Petroli toka 750 hadi 1800?
Shilingi toka 1000 hadi 1500 kwa dola moja?
Kununua magari ya viongozi ya milioni 200+?
Kufelisha karibu nusu ya wanafunzi wa kidato cha nne?
Kuzalishia mama zetu sakafuni na wagonjwa 3 kuchangia kitanda kimoja?
Kupeleka watoto India au Afrika Kusini kufanyiwa dialysis wakati machine zinauzwa dola 10,000?
Kuua Air Tanzania?
Kuwepo kwa foleni ya masaa 3 toka Kimara kwenda mjini?
Give me a freakin break!! Kujijengea makasri hapo Migombani Street sio kuongoza nchi.

Kwa utawala wa namna hiyo heri vijana wa Chuo Kikuu wangeweza kuongoza nchi hii kuliko hii serikali ya sasa. Kukopa hela na kuweka barabara kadhaa lami na nyingine changarawe ndio ingemshinda Lipumba?

No comments:

Post a Comment