Friday, October 22, 2010

MAMLAKA YA BUNGE YA KUMUONDOA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA CHINI YA IBARA YA 46A ya KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977.

Ibara ya 46A YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977; INAYOHUSU KUMUONDOA MADARAKANI (IMPEACHMENT) RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 [Cap. 2 R.E. 2002.] Leo hii Ijumaa 22/10/2010) - Somo la Katiba [Constitutional Law]

ZOEZI HILI HUCHUKUA JUMLA {KAMA KILA KITU KINAKWENDA SAWA - ceteris paribus} YA SIKU 150 au miezi mitano.

Rais (Mhimili wa Utawala) anaweza kuondolewa madarakani chini ya Ibara hii kwa tuhuma za aina nne:
- kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
- Kukiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi [Leadership Code]
- Kukiuka vipengele vilivyomo katika maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya Siasa yaliyotajwa katika Ibara ya 20 (2) ya Katiba, au
- Amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Ili kuanzisha mchakato huo inahitaji idadi ya asilimia 20 (20%) ya Wabunge waliopo wafikishe Notisi ya maandishi na kuiwasilisha kwa Spika. Siku 30 zipite kabla ya kikao cha kujadili hizo tuhuma:

2. Baada ya kupita hizo siku 30, MTOA HOJA ATAIWASILISHA BUNGENI.

-Aidha tuhuma zitupwe au
- Wapendekeze kuunda Kamati ya Kuchunguza tuhuma hizo.

3. Bunge litapiga kura ili iundwe Kamati ya Kuchunguza tuhuma hizo; lakini kura hizo lazima zifikie au zizidi theluthi mbili ya kura zote. Kama ndio,

4. Spika anatakiwa kutaja majina ya Kamati ya Uchunguzi chini ya Ibara ya 46A(4) ambao ni:
(a) Jaji Mkuu (Mwenyekiti)
(b) Jaji Mkuu wa Zanzibar
(c) Wajumbe saba wanaoteuliwa na Spika; kwa kuzingatia Kanuni za Bunge na Uwakilishi wa Vyama vya Siasa Bungeni.

Matokea ya No. 3 hapo juu chini ya Ibara 46A (5) ni kwamba

- RAis anasimamishwa kazi
- Vivyo Ibara ya 37 (3) inafanya kazi. (Edapo Rais hatakuwepo madarakani wakati huo)

Jambo hili la kumsimamisha kazi Rais litaendelea hadi hapo Spika atakapomfahamisha Rais juu ya matokeo ya uchunguzi uliofanywa [Ibara ya 46A (5)]

Na. 4 hapo juu Kamati inapewa siku 7 kukamilisha uchunguzi wake na kumpa fursa Rais ya kujieleza [Ibara ya 46A (6)]

Kamati ya uchunguzi inapewa siku 90 kukamilisha ripoti yake na kuiwasilisha kwa Spika.

Ibara ya 46A (8) - Spika anawasilisha Ripoti ya Uchunguzi kwa Bunge

Ibara ya 46A (9) - Bunge lenye idadi isiyopungua theluthi mbili litajadili Ripoti hiyo na kumpa Rais fursa ya kujieleza.

Bunge linatakiwa liibuke na aidha ya majibu yafuatayo:

(i) Kwamba tuhuma zimethibitishwa.
(ii) Kwamba Rais hafai kuendelea kufanya kazi
(iii) Kwamba Rais hafai kuwa Rais
(iv) Kwamba tuhuma hazikuthibitishwa.

Ibara 46A(10) - Baada ya hilo kufanyika, endapo ni (i) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatakiwa kuachia ngazi (resign) ndani ya siku tatu.

MCHAKATO HUO WOOOOTE ULIOTAJWA HAPO JUU UKIFUATAWA KAMA UNAVYOTOLEWA kisheria unatakiwa kumalizika ndani ya siku 150 sawa sawa na miezi 5 kamili.

JAMANI, HILI KWELI LINAWEZEKANA AU IBARA YA 46(A) ya Jamhuri ya Muungano wa TAnzania imewekwa kiini macho tu kwa sisi walalahoi wa Tanzania tuendelee kuota kwamba tukifanyikwa kinyume na Ibara hii basi rais ataendelea kupeta tu???????? Nasema hivi kwa sababu mchakato mzima ni mgumu na hauna mwelekea wa kufanikiwa hasa ikingatiwa idadi ya wabunge husika wa mchakato huu!!!!!!

TUANGALIE UTARATIBU WA MAMLAKA YA BUNGE KUMUONDOA MADARAKANI (REMOVAL) RAIS, PIA KWA SABABU HIZO HIZO HUKO KATIKA NCHI YA JAMHURI YA AFRIKA YA KUSINI (REPUBLIC OF SOUTH AFRICA)
Ifahamike wazi hapa kwamba Kumuondoa Rais kwa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania ni "impeachment" wakati katika Jamhuri ya Afrika ya Kusini ni "Removal". Haya ni maneno mawili tofauti japokuwa matokeo au hatima ya michakato yake ni moja; ya kumuondoa mtu madarakani.

Chini ya Katiba yao ya mwaka 1996; Sheria Na. 108 ya Jamhuri ya Afrika ya Kusini; Ibara ya 89 (1) inasema hivi Kiingereza:

"The National Assembly by a resolution adopted with a supporting vote of at least two thirds of its members, may remove the President from office only on the grounds of -

(a) a serious violation of the Constitution or the law;
(b) serious misconduct; or
(c) inability to perform the functions of office.

Tafsiri ya Kiswahili ya Ibara hiyo ni hii hapa:

"Bunge linaweza kumuondoa rais madarakani kwa kutoa Azimio litakayokubaliwa kwa kupigiwa kura na angalau theluthi mbili ya wabunge wote. Rais anaweza kuondolewa madarakani kwa sababu zifuatazo tu:
(a) Kosa kubwa la Kuvunja katiba ya nchi au sheria;
(b) Mwenendo unaodhalilisha [serious misconduct]
(c) Kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kazi ya ofisi hiyo.

Ibara ya 89 (2) inasema kwamba yeyote atakayeondolewa chini ya Ibara ya 89 (1) kutokana na sababu (a) au (b) anaweza kunyimwa mafao yote yaendanayo na ofisi hiyo; na pia anaweza kupoteza sifa ya kufanya kazi katika wadhifa mwingine wowote ya umma.

Vipengele hivi katika Katiba ya Jamhuri ya Afrika ya Kusini havitaji muda wowote kutoka kutolewa Azimio hadi kumuondoa madarakani. Kwa maneno mengine, jambo hilo linaweza kufanyika ndani ya muda mfupi iwezekanavyo.

Ibara ya 35 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Afrika Kusini, inayozungumzia haki za mshitakiwa inasema kila mtuhumiwa ana haki ya kupata kuhukumiwa ipasavyo; inayojumlisha haki ya:

(a) Kufahamishwa kosa lake kikamilifu ili aweze kujitetea
(b) Kupewa muda wa kutosha na nyenzo za kuweza kujitetea.
(d) Kupata haki ya kusikilizwa kwa wakati bila kucheleweshwa(zote hizi ni sehemu ya haki ya Kusikilizwa kikamilifu)

Kwa hiyo vipengele hivi vitatu vikifuatwa barabara, hata hivyo, nina hakika haitachukua siku 150 kwa shauri hilo kufikia tamati. Yawezekana pegine kuchukua mwezi mmoja au miwili, bila shaka kutegemea na shutuma zenyewe na uendeshaji wa kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment