HAYA NI MAJIBU JUU YA HABARI ILIYOTOKA KATIKA GAZETI LA NIPASHE LA TANZANIA LA IJUMAA, MEI 21, 2010, UKURASA WA TATU, ILIYOKUWA NA KICHWA CHA HABARI KISEMACHO "CHADEMA YADAI CCM IMEANZA KUCHEZA RAFU".
Mkurugenzi wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, TAMBWE HIZZA aliyesema "Tunahakikisha kila mwanachama wetu anajiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura ili siku ya uchaguzi apige kura na ambaye hatafanya hivyo hataruhusiwa kupiga kura za maoni ndani ya chama" (cha CCM) ni kauli ya kuivunja ibara ya 5 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa sababu zifuatazo:
1. Haki iliyotajwa ya kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania na ni haki ya hiari. Yawezekana mwananchi au raia hapendi kujiandikisha kupiga kura, hivyo halazimishwi kufanya hivyo, kulingana na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo kuiunganisha na kulazimisha haki ya kupiga kura chamani CCM na haki ya kujiandikisha kupiga kura ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kumnyima haki mwana-CCM katika uhuru wake wa kupiga kura katika kura za maoni.
Hata kama hiyo kanuni iliwekwa katika Katiba au Taratibu na Kanuni za CCM juu ya jambo hilo, chama hicho kinatakiwa kitambue kuwa kanuni au taratibu hiyo inavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, hivyo ifutwe mara moja Kanuni hiyo inayokwenda kinyume na Katiba yetu.
Sababu za au ZUIO la Mwananchi wa nchi hii kupiga kura zimeaorodheshwa katika Ibara ya 5 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Hivyo kigezo kinachosema lazima mpiga kura za Maoni ndani ya CCM awe na Kitambulisho cha kupiga kura sio moja la ZUIO ninalolizungumzia ndani ya Ibara ya 5 (2). Hivyo ni kumvunjia haki yake mwanachama wa CCM ya kupigia kura amtakaye katika kura za maoni katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu Octoba 30, 2010.
No comments:
Post a Comment