Saturday, May 16, 2015

KWA NINI VIUMBE HUJAMBA?

 SABABU  ZA  VIUMBE   KUJAMBA   NA   FAIDA  ZAKE
Imedakwa  Mtandaoni. 

Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka? Kujamba
inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu,lakini
inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo
la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda. Kila
mtu anajamba,hata Halle Berry   [she is also human - nae ni kiumbe pia] nae hujamba.

1.Kujamba ni nini hasa?

Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa,ambayo
inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi. Baadhi ni hewa
tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa. Hewa ingine
husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu
kutoka kwenye damu,na baadhi ya gesi huzalishwa na
kemikali katika utumbo au bakteria.Kwa kawaida
"ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya
nitrogen, asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni carbon
dioxide, asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oxygen.
Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen
sulfide na mercaptans,ambayo ndio ina sulfur ndani
yake, sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya
Kujamba huambatana na sauti,hii ni kutokana na
"vibration" katika njia ya haja kubwa.Ukubwa wa mlio wa
kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje
na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.

2.Kwa nini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?

Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa
mtu,vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio husababisha
hili.Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama
maharage, kabichi, soda na mayai.

3.Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku

Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa
siku.Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi
cha miaka 6, anaweza kuzalisha nishati ya kutosha
kutengeneza bomu la atomiki.

4.Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde.

Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada
ya mtu kujamba,hiyo ni kwa sababu inachukua muda
mrefu kwa harufu kufikia pua.

5.Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya Yako

Madaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia
kujamba ni hatari kiafya.  Baadhi ya wataalam wanafikiri
kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa
mmeng'enyo wa chakula, hivyo kujizuia kujamba
haitakuletea madhara.Wengine wanadhani kwamba
kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa
gesi,na pia inaweza sababisha bawasili (hemorrhoids).

6.Kwa Baadhi ya Tamaduni, Kujamba Sio Ishu [tatizo]

Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba
lifanywe kistaarabu,kuna baadhi ya tamaduni hawaoni
haya kujamba hadharani, na pia hufurahia tendo
hilo.Mfano kabila la Yanomami huko America ya
Kusini,kwao husalimiana kwa kujamba, na China
unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya
zamani,Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia
kujamba inaweza kuwa hatari kiafya, alipitisha sheria
kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".

7.Ushuzi Unawasha Moto

Kama ilivyoandikwa hapo juu, methane na hydrogen
inayozalishwa na ushuzi inaweza sababisha moto.

8.Mchwa Hujamba Kuliko Wanyama Aina Zote

Ni ngumu kuamini kuwa mchwa ndo anawajibika na
matatizo yetu ya "Global Warming".Mchwa huongoza kwa
kujamba kwa wanyama, na hivyo huzalisha gesi ya
methane.

9.Ukiubana Ushuzi, Utakutoka Usingizini

Hata ujitahidi kuubana vipi, ushuzi utatoka mara
utapokua umepumzika, hasa ukiwa umelala.

10. Watu Hujamba Hata Baada ya Mauti Kuwafika

Maiti huendelea kutoa gesi hadi masaa matatu baada ya
mtu kufariki dunia, hii huambatana na milio ya
kujamba. Hali hii husababishwa na misuli kusinyaa.

UKIPATA NAFASI JAMBA MWANANGU😜😜😜😜 NI AFYA,  NI   MAUMBILE !!!!

No comments:

Post a Comment