Wednesday, April 22, 2015

UKATILI WA WAAFRIKA DHIDI YA WAAFRIKA NCHINI AFRIKA KUSINI


 YAMECHANGIWA  NA  VIBARAKA  WA  INKATHA,  KWAZULU NATAL

Jamani naomba niwaambie kuwa Wazulu hawakunyanyaswa na apartheid kwani kule Kwa Zulu Natal kulikuwa hakuna apartheid kwan waliachwa wajitawale na Mfalme wao pia Waziri wao Mkuu alikuwa ni Mangosuthu Buthelezi chini ya chama chao cha Inkatha Freecom Party.

Ni watu wachache sana katika Wazulu ndio walijiunga na ANC kama Zuma nakupiga vita ya ukumbozi.

Kwa kiasi kikubwa Wazulu walikuwa vibaraka. Hivyo mnaposema kuwa mliwasaidia Waafrika Kusini wajikomboe ni upuuzi kwa Wazulu kwani wao walitaka apartheid iendelee.

Pia Wazulu kule kwao hata wakati wa Mandela ANC huwa haishindi. Hata Zuma alipogombea ubunge kule kwao alishindwa. Pia muelewe kuwa hata Mandela alipoachiwa huru hao Wazulu chini ya chama chao cha Inkatha waliingia barabarani na kuwaua watu wa makabila mengine na hasa watu wa ANC.

Palitokea machafuko makubwa sana ya Wazulu kuwaua watu weusi wenzao kwani hao Wazulu hawakupenda apartheid iishe. Makaburu miaka yote walikuwa wanawatumia Wazulu kuwaua watu wengine weusi.

Pia mkumbuke kuwa mchakato wa katiba ya Afrika Kusini ile ya mwaka 1994, hao wazulu chini ya Buthelezi wao walisusia bunge la katiba kama UKAWA walivyofanya hapa Tanzania baada ya kuona hoja zao zitashindwa kwani wao Wazulu walitaka serikali za majimbo zipewe mamlaka kamili.

Hata Mandela alishindwa kuwashawishi warudi ila walibanwa na mataifa ya magharibi wakarudi ila hoja zao zilishindwa. Pia muelewe kuwa hao Wazulu huwa hawaichagui ANC hata wakati wa Mandela. Wakati wa kupitisha katiba ya Afrika Kusini, ANC ilihitaji 2/3 ya wabunge wote  ambayo ni kama 66% ya wabunge wakati ANC wakati huo wa Mandela ilikuwa na 63% ya wabunge wote hivyo wabunge wa Wazulu kama wanne hivi wakatoa maamuzi ya kuwaunga ANC ndio katiba ikapita bila hivyo nchi hiyo isingekuwa na katiba na vita ingetokea.

Pia sababu ya Mandela kutaka Zuma awe Rais wa Afrika Kusini ni kwa sababu Wazulu hawapendi umoja wa taifa na pia kwa vile Zuma aliiacha yote kwani hata Wazulu walitaka kumuua kwa kutaka Afrika Kusini iwe mmoja.

Zuma ni kawa mtu wa Pemba ambaye Pemba yote ipo CUF ila Mpemba mmoja (Dr. Shein) ambaye huko kwao Pemba katengwa lakini kabaki CCM.

Pia Wazulu wanamsikiliza mfalme wao kuliko raisi wa nchi. Pia Wazulu kuuwa ni jambo la kawaida, na kutetea maslahi ya kabila ni jambo jema kuliko kutetea nchi. Wazulu wanapenda wawe na serikali yao kama kabla ya, na wakati wa apartheid.

Nimeamua niandike hivi ili muelewe kuwa Wazulu kuwapinga wageni ni jambo jema kwa wazulu. Pia huyo mfalme wao anashirikiana na makaburu mpaka leo hii ndio maana mfalme aliposema tu wageni warudi kwao na mauaji yakaanza. Hata baadhi ya haya niliyoyaandika mkisoma "Long Walk to Freedom" ya Mandela ameandika pia, na pia nawashauri msome vizuri historia ya Afrika.

Ukabila bado utaisumbua Afrika kwa muda mrefu sana. Pia viongozi vibaraka bado wapo Africa. Tena hawa Wazulu wakimaliza kuwaua watu wasiokuwa wa-Afrika Kusini kisha wataanza kuwaua wale wa Afrika Kusini ambao siyo Wazulu.

Pia mjue kwa Wazulu wengi Mandela siyo shujaa wao kwani Wazulu walitaka apartheid iendelee kwa kuwa walipewa hata ruzuku kutoka kwa makaburu.

Hiki chama cha Inkatha kina wabunge 10 kwa sasa kati ya wabunge 400 wa Afrika Kusini yote. Na sera za Inkatha hadi leo ni utawala huru wa majimbo na kupendelea kabila lao. Unaweza ukajua hapa Tanzania ni chama gani kinataka utawala wa majimbo na kina sura na umbile la kikabila kama Inkatha.

Hivyo siyo sahihi kusema tuliwasaidia wa-Afrika Kusini kudai uhuru mbona wanafukuza Waafrika wenzao? Mnapaswa mjue kuwasaidia Afrika Kusini iwe huru ilikuwa ni dhambi kwa wale Wazulu. Waafrika wengi walio Afrika Kusini ni wa Malawi ambao wengi wanafanya domestic works na hospitality industry wengine ni wa Mozambique. Na wa Somali pia ambao wanafanya kazi za hatari kama kuzoa taka, kuzibua vyoo, etc.

Nchi nyingine hazina raia wengi pale Afrika Kusini. Hizi nchi zinatuzunguka nyingi niliwahi zifanyia kazi maalum yaani nazifahamu vizuri sana. Pia hata hapo Kwa-Zulu Natal ni watu wachache sana ambao wanaunga mkono Inkatha na ubaguzi wao sio wengi kwani ANC ilipata viti vingi hata serikali ya mkoa wa Kwa-Zulu Natal ANC ina viti nadhani 52 dhid ya 80, Inkatha ni wanafiki, wakabila, wabaguzi.

No comments:

Post a Comment