Tuesday, July 24, 2012
BARUA KWA MUFTI WA BAKWATA KUHUSU MAHAKAMA YA KADHI TANZANIA
1
سم لله الرحمن الرحيم
WAJUMBE WA JOPO LA MASHEIKH
MCHAKATO WA MAHAKAMAA YA KADHI
Kumb. Na WJM/BKT/01/2012 29 Shaaban, 1433
17 Julai, 2012
Kwa: Mufti Sheikh Issa bin Shaaban,
MUFTI WA BAKWATA,
S.L.P
DAR ES SALAAM.
لیكم و رحمة لله, السلام
YAH: KWENDA KINYUME NA JOPO LA MASHEIKH
Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.
Sisi masheikh tulioorodhesha majina yetu hapa chini, ambao ni wajumbe
katika Jopo la Msheikh 25 wa taasisi na jumuiya mbali mbali zilizosajiliwa
kisheria ambalo tangu liundwe limekuwa katika mazungumzo na serikali
kuhusu suala la urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini, tumepokea
habari kwamba umeteua Kadhi Mkuu, manaibu wake wawili na makadhi wa
mikoa kwa mshangao mkubwa na tungependa ufahamu kwamba.
Mosi, maamuzi yako ya kuteua makadhi wakati suala hili lilikuwa bado
halijafikia hitimisho, ni maamuzi batili kwa mujibu wa mafundisho ya
Uislamu, hadidu rejea za Jopo, sheria za nchi na pia hata uhalisia wa mambo
tu ulivyo kuhusu suala hili.
Pili, maamuzi yako yamemfanya Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania aonekane si mkweli kwa sababu kwa muda wote wa
miaka miwili amekuwa akimfamhamisha Mhe. Rais, wabunge, waislamu na
watanzania kwa ujumla kwamba kuna mazungumzo kati ya kamati ya
masheikh na serikali na mara ya mwisho kikao cha kamati hiyo na Waziri
Mkuu kilifikia hatua ambazo utekelezaji wake ndio ungetoa picha waislamu
wanaanzishaje Mahakama ya Kadhi nchini.
2
Tatu, Kadhi Mkuu na Makadhi uliowateua si makadhi wa Mahakama ya Kadhi
tunayoipigania muda wote huu kwa sababu bado Mahakama ya Kadhi
haijaundwa kwa mujibu wa makubaliano ya kikao chetu cha mwisho na
Waziri Mkuu na pia ki-Shariah na ki-Sheria hauna mamlaka ya kuwateulia
waislamu wote nchini makadhi.
Kutokana na mas’ala hayo matatu tuliyoyataja hapo juu, tunataka ufanye
yafuatayo kwa maslahi ya Uislamu;-
i) Utangaze kwamba umekosea kwa kukiuka mojawapo ya hadidu rejea
za jopo na kwamba Makadhi uliowateua si makadhi wa Mahakama ya
Kadhi ambayo waislamu tunaipigania kwa muda wa miaka kadhaa
sasa na ambayo Jopo la Masheikh tulikubaliana tangu mwanzo wa
mchakato huu wa Mahakama ya Kadhi baina ya waislamu na serikali
na uainishe kwamba hao ni makadhi wa Bakwata na si makadhi wa
waislamu wote.
ii) Uwauzulu mara moja makadhi wote uliowatangaza kwa maamuzi
yako binafsi pasina kuwashirikisha masheikh wote wa Jopo la
Masheikh 25 ambalo ndilo linalotambulika na serikali kuwakilisha
waislamu wote nchini. Kwa mujibu wa hadidu rejea, tulikubaliana
kwamba “mtu yeyote katika jopo la Masheikh 25 hapaswi kusema
lolote lile ambalo halina maamuzi ya pamoja ya wajumbe wa Jopo”.
iii) Uitishe kikao cha haraka cha Jopo la Masheikh 25 ndani ya siku saba
kuanzia tarehe ya kupokea barua hii vinginevyo tutautangazia
ummah kwamba hatuna imani na wewe kuongoza mchakato huu na
tutachukua hatua stahiki kukabiliana na udikteta huu.
iv) Kwa kuwa umeonesha kutoa maamuzi ya kidikteta, katika kikao cha
kwanza tu cha Jopo la masheikh 25 kitakachoitishwa ndani ya wiki
moja tuliyoitaja hapo juu, kitachagua Makamu M/Kiti, Naibu Katiba
na kuhakikisha kwamba ummah wa waislamu nchini unahusishwa
ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa taasisi zitakazoshiriki katika
kadhia hii ya Mahakama ya Kadhi.
3
Wabillahi Tawfiiq,
Signed
M/Kiti wa Kamati Ndogo ya Jopo la Masheikh
WAJUMBE WAFUATAO WAMESAINI KUUNGA MKONO MSIMAMO HUU
Names and signatures omitted on purpose
Nakala kwa:
1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ikulu,
Dar es Salaam.
2. Waziri Mkuu,
Ofisi ya waziri Mkuu,
Ikulu,
Dar es Salaam.
3. Spika wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
Dar es Salaam.
4. Waziri wa Katiba na Sheria
Wizara ya Katiba na Sheria
Dar es Salaam.
5. Mwanasheria Mkuun wa Serikali,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,
Dar es Salaam.
6. Mhe Jaji Mkuu,
4
Mahakama Kuu ya Tanzania.
7. Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa,
Dar es Salaam.
8. Jumuiya na Taasisi zote za Kiislamu Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment