Wednesday, November 18, 2009

KIINI CHA KUANZISHWA KWA UMOJA WA VIJANA WA TANU TANGANYIKA!

Nilitaka nikumegee kipande cha kitabu cha SIMBA WA VITA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA - RASHIDI MFAUME KAWAWA kilichotungwa na John M J Magotti. Kuna sehemu mwandishi anatueleza undani wa TYL.

Lo and behold, Banisraeli nikawakuta tena lakini kwa nini tuandikie mate? (page 43):

Kuanzishwa kwa Umoja wa Vijana wa TANU



Muasisi wa Umoja wa Vijana wa TANU alikuwa ni Kawawa. Mwaka 1958, Kawawa pamoja na Mwalimu Nyerere walihudhuria sherehe za Ghana kutimiza mwaka mmoja wa Uhuru (1958). Katika kuhudhuria sherehe hiyo wote wawili walipata fursa ya kukutana na Bi. Golda Meir ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel . Bi. Golda Meir aliwaeleza jinsi Israel ilivyokuwa ikiwaandaa vijana wake. Utaratibu wa Israel wa kuwaandaa vijana ulimvutia sana Mwalimu Nyerere na Kawawa. Waliporejea nyumbani, Mwalimu alimpa jukumu Kawawa la kuwaandaa vijana kama vile Isrel ilivyokuwa ikiwaandaa vijana wake.



Kawawa alianzisha rasmi Umoja wa Vijana wa TANU mwaka 1958. Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja Vijana ulimchagua Kawawa kuwa Mwenyekiti wao wa kwanza. Kabla ya kuanzisha Umoja wa Vijana wa TANU, Vijana walikuwa wamejiunga katika vikundi mbali mbali, kama vile, Watoto wa TANU, Bantu Group na Vijana wa TANU na "Station Group" ya Tanga ambacho baadaye kilibadili jina na kuwa TANU Volunteer Corps. Baada ya kuundwa kwa Umoja wa Vijana wa TANU, vikundi vyote hivi vikatoweka kwa maana kwamba nafasi ya vikundi hivyo ilichukuliwa sasa na Umoja wa Vijana wa TANU.



Hawa Vijana wa TANU ndiyo walikuwa wa kwanza kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ilipoanzisliwa mwaka 1964. Tanzania iliendelea kujifunza kwa Waisrael masuala yahusuyo vijana JKT ilipoanzishwa baadhi ya vijana wa Umoja wa Vijana wa TANU walipelekwa mafunzoni Israel kwa lengo kwamba ya kuhitimu mafunzo yao ndiyo wangekuwa wakufunzi katika Jeshi In Taifa na hivyo ndivyo ilivyokuwa

No comments:

Post a Comment