Wednesday, December 31, 2008

THE NATIONAL MUSEUM OF AMERICAN INDIANS

Leo Jumanne, tarehe 30 Disemba, 2008, nimetembelea Makumbusho ya "The National Museum of the American Indian" yaliyopo Independence Avenue, Washington DC. Makumbusho haya ni muhimu sana ya wenye asili ya Bara hili la Amerika. Nia na madhumuni yangu hasa nilitaka kuona na kujua endapo kuna mambo yeyote yale ambayo yanaweza kuwa yanafanana kati ya utamaduni wa watu hawa na watu waliopo Afrika.

Kwa kweli nilikuta mengi ya kupendeza. Kwa upande wa kupamba na kutengeneza vitambaa (weaving) hatuwawezi. Ni mahodari sana.

Nimeona jinsi wenzetu walivyokuwa na silika za kuongozwa na machifu kama sisi, nimeweza kuona pia asili ya kutumia mawe katika kutengeneza silaha za kale kama mishale na mikuki ya kuvulia samaki na kuwindia wanyama wengine. Pia nimeona wana asili ya kutumia mawe kusagia unga wa mahindi, ambacho ndio kwao pia ni chakula kikuu. Mahindi yao yana rangi mbalimbali tofauti na ya Afrika. Wana utamaduni pia wa kufinyanga vyungu kwa kutengenezea vifaa vya nyumbani.

No comments:

Post a Comment