Monday, December 29, 2008

Mlamwassawaukae.blogspot

Watanzania wenzangu na kadamnasi yote iliyopo, itakayokuja na inayoelewa lugha hizi; yaani ya Kiswahili na Kiingereza; leo Jumatatu, Disemba 29, 2008,nawakaribisha sana katika ukumbi huu tusaidiane kuelimishana, kukumbushana na kufahamishana masuala ya maisha yetu ya kila siku hapa duniani.

Ni matarajio yangu kuwa mtapata fursa ya kutembelea ukumbi huu, na kuchangia mambo ya manufaa kwa ajili yetu, ya kizazi chetu na vizazi vitakavyokuja baadaye.

Midhali elimu haina mwisho, tusichoke kuelimishana yenye manufaa kwetu sote, nasi tujitolee kuelimisha kwa chochote tunachokifahamu na tunachoamini kuwa kitamsaidia binadamu mwingine. Karibuni sana na Mungu awabariki kwa michango yenu.

5 comments:

  1. KWELI Elimu haina mwisho. Leo hii Jumatatu, tarehe 29 Disemba, 2008 nimefanikiwa kufungua blogu hii nikiwa katika pilika za mihangaiko ya Elimu ya Watu Wazima. Jitihada zangu za kufahamu namna ya kuanzisha blogu zimefanikiwa na matokeo ndio haya hapa. Karibuni.

    5167 Fulton Str. NW,
    Washington DC. 20016,
    U.S.A.

    ReplyDelete
  2. Tarehe 31 Oktoba, 2008 nikiwa shuleni, nikahitaji kuingia maliwatoni. Nikiwa huko nanawa mikono, akaingia mhitaji mwingine, Mama wa Kimarekani mweupe na mtoto ndani ya kigari chake cha kusukuma.

    Kwa mazoea ya utamaduni wetu wa Kiafrika, nilidhani yule mama ataniomba nimshikie au nikae na mtoto wake akiwa humo humo ndani ya kigari chake cha kusukuma, ili akajisaidie. Kumbe Wamarekani hawamwamini binadamu mwenzao. Yule mama akaingia na mtoto wake ndani ya kigari hadi chooni! Nilibaki hoi! Jamani tembea uone!

    ReplyDelete
  3. Hongera kwa kuanzisha ukumbi huu. Nakutakia mafanikio katika yote uliyoelezea hapa juu.

    ReplyDelete
  4. Karibu sana! tena sana! Nafurahi kuifahamu blogu yako na kusoma habari unazobandika.

    ReplyDelete