Sunday, April 14, 2013

FAIDA ZA MTI WA MLONGE [MORINGA]

 Imedakwa toka mitandaoni, leo hii 14 Aprili, 2013.

 FAIDA  ZA  MTI  WA  MLONGE  [MORINGA]

KAMA kuna mti wenye faida nyingi za kiafya, basi Mlonge unaweza kuwa unaongoza. Kila eneo la mti huu, kuanzia majani, maua, mbegu, magamba  hadi mizizi yake ina virutubisho vya kipekee vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu.

Majani ya Mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wake unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika moja lijulikanalo kama Trees For Life, majani ya Mlonge yana Vitamin A nyingi kuliko karoti, vitamin C nyingi kuliko machungwa na madini ya Potassium nyingi kuliko ndizi mbivu, halikadhalika ubora wa protini yake ni bora kushinda maziwa na mayai.

Kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini ya chuma  (Iron), kasiamu (Calcium) na vitamin nyingi za aina mbalimbali, majani ya mmea huu yamekuwa yakitumika kama ‘tonic’ kwa watoto wadogo na vijana ili kuimarisha mifupa na kusafisha mfumo wa damu mwilini.

Ili kutengeneza ‘tonic’, saga majani mabichi ya Mlonge pamoja na maji, yachuje kisha changanya na maziwa halisi. Inaelezwa kuwa juisi ya aina hii ni dawa nzuri kwa waja wazito, kwani huboresha njia ya uzazi na kumuwezesha mama kuzaa bila matatizo na kuondoa matatizo baada ya kujifungua.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, mti wa Mlonge unatibu karibu magonjwa 300 ya aina mbalimbali, yakiwemo yale magonjwa sugu, baadhi yake ni kama haya yafuatayo:

Mlonge unaweza kutibu Pumu, Kikohozi na Kifua Kikuu. Aidha, magonjwa mengine kama Kisukari, Shinikizo la damu (la juu na chini), magonjwa ya ngozi, magonjwa ya kwenye njia ya mkojo (UTI) kuongeza kinga ya mwili (CD4) na kuongeza nguvu za kiume.

1 comment:

  1. I've got nothing left to say. "ahsante kwa maelezo yako mazuri".

    ReplyDelete